CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025: Term One Opener Assessment 2025 (Set 3)
Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 38 questions
Topics: Kusoma, Kuandika, Sarufi na Matumizi ya Lugha.
All 38 questions with answers
- Question 1: Kwa nini Mzee Mati alipata mazao mengi kila msimu? (alama 1)Answer: Kwa sababu alizingatia mbinu bora za kilimo.
- Question 2: Ni jambo lipi linaloonyesha kuwa Mzee Mati aliwajali wanyama? (alama 1)Answer: Baada ya kuvuna alibakisha mazao kiasi shambani na kuwaacha wanyama waingie shambani kuyala bila kuwazuia.
- Question 3: Unafikiria ni kwa nini nyani waliandaa sherehe? (alama 1)Answer: Walifurahi kwamba Mzee Mati, waliyemchukulia kama adui, ameugua; walidhani hangeweza kuvuna wala kuwafukuza,…
- Question 4: Andika funzo moja linalojitokeza katika hadithi hii. (alama 1)Answer: Tusiwadharau watu wanaotusaidia hata kama msaada wao ni mdogo, kwa sababu baniani mbaya kiatu chake dawa.
- Question 5: Uzalendo ni nini? (alama 1)Answer: Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda nchi yake.
- Question 6: Mzalendo hufanya mambo yote haya isipokuwaAnswer: B. kutetea mila potovu na uhalifu
- Question 7: Andika njia moja ambayo wewe binafsi unaweza kuonyesha uzalendo. (alama 1)Answer: Kuwasaidia watu wenye shida bila kujali dini, kabila wala rangi yao.
- Question 8: Neno 'nia' limetumika katika kifungu. Kisawe cha neno hilo niAnswer: A. Lengo
- Question 9: Andika habari kuu iliyoangaziwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Answer: Taifa haliwezi kuendelea iwapo mchango wa baadhi ya wanajamii, kama akina mama, vijana na watu wenye…
- Question 10: Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 10. (alama 1)Answer: Wanawake wana uwezo wa kuleta maendeleo kama wanaume.
- Question 11: Andika ujumbe wa aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Answer: Kila mtu apewe nafasi kulingana na uwezo wake na si maumbile yake.
- Question 12: Ipe habari hii kichwa kifaacho. (alama 1)Answer: Mchango wa Kila Mwanajamii katika Maendeleo
- Question 13: Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 13.Answer: D. yameuwezesha
- Question 14: Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 14.Answer: A. huwasiliana
- Question 15: Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 15.Answer: C. walipo
- Question 16: Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 16.Answer: B. marefu
- Question 17: Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 17.Answer: D. almradi
- Question 18: Chagua kadi iliyo na nomino za makundi pekee.Answer: A. Shada, jamii, kikosi
- Question 19: Karani alikuwa akiandika barua. Iandike sentensi hii katika wakati ujao hali ya kuendelea. (alama 1)Answer: Karani atakuwa akiandika barua.
- Question 20: Chagua kitenzi kisaidizi katika sentensi hii. Mtoto huyu huwa anawatii wazazi wake. (alama 1)Answer: huwa
- Question 21: Kamilisha kwa kutumia ndi-. Sisi ... tuliopanda miti ile. (alama 1)Answer: Sisi ndisi tuliopanda miti ile.
- Question 22: Andika wingi wa sentensi ifuatayo. Bawabu ameufunga mlango vizuri. (alama 1)Answer: Mabawabu wameifunga milango vizuri.
- Question 23: Kamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi. ... yao haina ... lolote. (doa, ndoa) (alama 1)Answer: Ndoa yao haina doa lolote.
- Question 24: Kanusha sentensi hii. Maji ya kunywa yalichemshwa. (alama 1)Answer: Maji ya kunywa hayakuchemshwa.
- Question 25: Andika kauli ya kutendwa ya sentensi ifuatayo. Sogora ameicheza ngoma hii vizuri. (alama 1)Answer: Ngoma hii imechezwa vizuri na sogora.
- Question 26: Badili sentensi ifuatayo iwe katika hali ya ukubwa. Alimwona nyoka mkubwa katika shamba lake. (alama 1)Answer: Alimwona joka kubwa katika jamba lake.
- Question 27: Geuza sentensi ifuatayo iwe katika usemi wa taarifa. “Mkutano utafanyika hapa kesho,” chifu aliwaambia wakazi. (alama 1)Answer: Chifu aliwaambia wakazi kwamba mkutano ungefanyika pale siku iliyofuata.
- Question 28: (a) Wimbo huu ni wa aina gani? (alama 1)Answer: Ni wimbo wa watoto (wimbo wa michezo ya watoto).
- Question 29: (b) Eleza mazingira ambamo nyimbo za aina hii huimbwa. (alama 1)Answer: Huimbwa na watoto wanapocheza pamoja nje, k.m. uwanjani nyumbani jioni au mbalamwezi, au shuleni wakati wa…
- Question 30: (c) Fafanua sifa tatu za nyimbo za aina hii zinazojitokeza katika wimbo huu. (alama 3)Answer: Una maswali na majibu: "Jina lako nani" – "Jina langu Pendo". Una takriri: "yoyoyo" na "tikisa bega, tikisa…
- Question 31: (d) Nyimbo za aina hii ni muhimu katika jamii. Andika mifano miwili ya umuhimu huo. (alama 2)Answer: Huwaburudisha watoto. Huwapa watoto mazoezi ya mwili wanapocheza.
- Question 32: (e) Wimbo huu ni mfano wa aina gani ya fasihi? (alama 1)Answer: Fasihi simulizi.
- Question 33: (f) Taja wahusika wawili katika wimbo huu. (alama 2)Answer: Pendo na Lulu.
- Question 34: Andika aina mbili za mandhari yanayojitokeza katika dondoo hii. (alama 2)Answer: Ukumbi wa mahafali katika chuo kikuu cha Umma University; kijijini Kajificheni (shamba la mibuni).
- Question 35: Dondoo hii imeshughulikia masuala mbalimbali. Fafanua masuala yoyote mawili kati ya hayo.Answer: Elimu: Subira alisoma kwa bidii hadi akapata shahada ya uzamili. Dhuluma: baada ya kifo cha baba, ami zao…
- Question 36: Eleza sifa mbili za Subira kulingana na dondoo hii. (alama 2)Answer: Ni mwenye bidii: alitia chudi masomoni akapata matokeo bora. Ni mwenye shukrani: anakumbuka juhudi za mama…
- Question 37: Hatufai kukata tamaa kwa sababu ya changamoto za maisha. Jadili kauli hii ukirejelea mfano wa mamaye Subira. (alama 2)Answer: Baada ya baba kufariki na ami kuwafukuza, mama hakukata tamaa: alihamia mjini akafanya biashara ndogondogo…
- Question 38: Mwandishi wa dondoo hii ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Huku ukitolea mifano mwafaka, eleza mbinu zozote tatu kati ya hizo. (alama 3)Answer: Tanakali za sauti: "Machozi yalimdondoka ndo ndo ndo!" Tashbihi: "tuliishi kwa furaha mithili ya mfalme…