CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 10
Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 10. (alama 1)
From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho
UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Taifa haliwezi kuendelea iwapo mchango wa baadhi ya wanajamii utapuuzwa. Serikali za mataifa mengine hupuuza mchango wa akina mama, vijana na watu wenye mahitaji maalum. Hali hiyo huweza kuchangiwa na ubaguzi, mila potovu au hata udikteta.
Watu wa jinsia ya kike wana uwezo wa kuleta maendeleo kama ilivyo kwa wanaume. Wanaweza kushiriki katika uongozi, ufundi, kilimo na nyanja nyingine zote za kiuchumi. Kupuuza mchango wa akina mama ni sawa na kufanya kazi kwa mkono mmoja huku mwingine umeutia mfukoni.
Wakati umefika ambapo kila mmoja anafaa kupewa nafasi kulingana na uwezo wake bali si maumbile yake. Wakati mwingine maumbile hutudanganya tukawapa nafasi wale wasio na uwezo unaohitajika huku tukikosa kuwashirikisha wale ambao wangetusaidia kupiga hatua.
10. Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 10. (alama 1)
Answer
Wanawake wana uwezo wa kuleta maendeleo kama wanaume.
Aya ya pili inasema watu wa jinsia ya kike wana uwezo wa kuleta maendeleo kama wanaume, hivyo mchango wao usipuuzwe.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Andika ujumbe wa aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11
- Ipe habari hii kichwa kifaacho. (alama 1)Question 12
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 14.Question 14
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 15.Question 15
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 16.Question 16