CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 9
Andika habari kuu iliyoangaziwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)
From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho
UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Taifa haliwezi kuendelea iwapo mchango wa baadhi ya wanajamii utapuuzwa. Serikali za mataifa mengine hupuuza mchango wa akina mama, vijana na watu wenye mahitaji maalum. Hali hiyo huweza kuchangiwa na ubaguzi, mila potovu au hata udikteta.
Watu wa jinsia ya kike wana uwezo wa kuleta maendeleo kama ilivyo kwa wanaume. Wanaweza kushiriki katika uongozi, ufundi, kilimo na nyanja nyingine zote za kiuchumi. Kupuuza mchango wa akina mama ni sawa na kufanya kazi kwa mkono mmoja huku mwingine umeutia mfukoni.
Wakati umefika ambapo kila mmoja anafaa kupewa nafasi kulingana na uwezo wake bali si maumbile yake. Wakati mwingine maumbile hutudanganya tukawapa nafasi wale wasio na uwezo unaohitajika huku tukikosa kuwashirikisha wale ambao wangetusaidia kupiga hatua.
9. Andika habari kuu iliyoangaziwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)
Answer
Taifa haliwezi kuendelea iwapo mchango wa baadhi ya wanajamii, kama akina mama, vijana na watu wenye mahitaji maalum, utapuuzwa.
Aya ya kwanza inaanza na wazo lake kuu: taifa haliendelei likipuuza mchango wa baadhi ya wanajamii.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 10. (alama 1)Question 10
- Andika ujumbe wa aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11
- Ipe habari hii kichwa kifaacho. (alama 1)Question 12
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 14.Question 14
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 15.Question 15