CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 8
Neno 'nia' limetumika katika kifungu. Kisawe cha neno hilo ni
From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.
Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda nchi yake. Raia wakiwa wazalendo kindakindaki huwa tayari kuipigania nchi yao kwa jino na ukucha. Yeyote anayejaribu kulidhalilisha taifa lao huwa adui kwao. Wao humpinga kwa maneno na matendo.
Vijana wanaweza kudhihirisha uzalendo wao kwa njia nyingi. Kwanza ni kuzingatia maadili muhimu kama vile upendo, umoja, heshima kwa wengine, ukarimu na uwajibikaji. Wakimwona mtu yeyote akiwa na shida, wamfae bila kujali dini, kabila wala rangi yake.
Halikadhalika, vijana wanapaswa kuungana katika kupiga vita maovu ya kijamii. Haya ni pamoja na mila potovu, unyanyasaji, matumizi ya mabavu na visa vyote vya ukiukaji wa sheria. Wawe wenye nia thabiti ya kukomesha uozo wote wa kijamii.
8. Neno 'nia' limetumika katika kifungu. Kisawe cha neno hilo ni
- ALengo
- BWajibu
- CSababu
- DMbinu
Answer
A. Lengo
"Wawe wenye nia thabiti ya kukomesha uozo" maana yake ni wawe na lengo (azma) thabiti. Kisawe cha nia ni lengo.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Andika habari kuu iliyoangaziwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Question 9
- Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 10. (alama 1)Question 10
- Andika ujumbe wa aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11
- Ipe habari hii kichwa kifaacho. (alama 1)Question 12
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 14.Question 14