naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 11

Andika ujumbe wa aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)

From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho

UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

Taifa haliwezi kuendelea iwapo mchango wa baadhi ya wanajamii utapuuzwa. Serikali za mataifa mengine hupuuza mchango wa akina mama, vijana na watu wenye mahitaji maalum. Hali hiyo huweza kuchangiwa na ubaguzi, mila potovu au hata udikteta.

Watu wa jinsia ya kike wana uwezo wa kuleta maendeleo kama ilivyo kwa wanaume. Wanaweza kushiriki katika uongozi, ufundi, kilimo na nyanja nyingine zote za kiuchumi. Kupuuza mchango wa akina mama ni sawa na kufanya kazi kwa mkono mmoja huku mwingine umeutia mfukoni.

Wakati umefika ambapo kila mmoja anafaa kupewa nafasi kulingana na uwezo wake bali si maumbile yake. Wakati mwingine maumbile hutudanganya tukawapa nafasi wale wasio na uwezo unaohitajika huku tukikosa kuwashirikisha wale ambao wangetusaidia kupiga hatua.

11. Andika ujumbe wa aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)

Answer

Kila mtu apewe nafasi kulingana na uwezo wake na si maumbile yake.

Aya ya mwisho inasema wakati umefika ambapo kila mmoja anafaa kupewa nafasi kulingana na uwezo wake bali si maumbile yake.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test