naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 6

Mzalendo hufanya mambo yote haya isipokuwa

From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.

Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda nchi yake. Raia wakiwa wazalendo kindakindaki huwa tayari kuipigania nchi yao kwa jino na ukucha. Yeyote anayejaribu kulidhalilisha taifa lao huwa adui kwao. Wao humpinga kwa maneno na matendo.

Vijana wanaweza kudhihirisha uzalendo wao kwa njia nyingi. Kwanza ni kuzingatia maadili muhimu kama vile upendo, umoja, heshima kwa wengine, ukarimu na uwajibikaji. Wakimwona mtu yeyote akiwa na shida, wamfae bila kujali dini, kabila wala rangi yake.

Halikadhalika, vijana wanapaswa kuungana katika kupiga vita maovu ya kijamii. Haya ni pamoja na mila potovu, unyanyasaji, matumizi ya mabavu na visa vyote vya ukiukaji wa sheria. Wawe wenye nia thabiti ya kukomesha uozo wote wa kijamii.

6. Mzalendo hufanya mambo yote haya isipokuwa

  1. Akupinga matendo ya watu wanaoharibu taifa
  2. Bkutetea mila potovu na uhalifu
  3. Ckuwafaa watu walio na mahitaji
  4. Dkupiga vita maovu ya kijamii

Answer

B. kutetea mila potovu na uhalifu

Kifungu kinasema vijana wazalendo hupiga vita mila potovu na ukiukaji wa sheria; hawazitetei. Mengine yote yametajwa kuwa matendo ya mzalendo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test