naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 5

Uzalendo ni nini? (alama 1)

From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.

Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda nchi yake. Raia wakiwa wazalendo kindakindaki huwa tayari kuipigania nchi yao kwa jino na ukucha. Yeyote anayejaribu kulidhalilisha taifa lao huwa adui kwao. Wao humpinga kwa maneno na matendo.

Vijana wanaweza kudhihirisha uzalendo wao kwa njia nyingi. Kwanza ni kuzingatia maadili muhimu kama vile upendo, umoja, heshima kwa wengine, ukarimu na uwajibikaji. Wakimwona mtu yeyote akiwa na shida, wamfae bila kujali dini, kabila wala rangi yake.

Halikadhalika, vijana wanapaswa kuungana katika kupiga vita maovu ya kijamii. Haya ni pamoja na mila potovu, unyanyasaji, matumizi ya mabavu na visa vyote vya ukiukaji wa sheria. Wawe wenye nia thabiti ya kukomesha uozo wote wa kijamii.

5. Uzalendo ni nini? (alama 1)

Answer

Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda nchi yake.

Sentensi ya kwanza ya kifungu inaeleza maana ya uzalendo.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test