CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 4
Andika funzo moja linalojitokeza katika hadithi hii. (alama 1)
From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 4.
Katika kijiji cha Maendeleo aliishi Mzee aliyeitwa Mati. Mzee huyo alikuwa na shamba kubwa. Alikuza maboga, matunda na nafaka mbalimbali katika shamba hilo. Msimu baada ya msimu, shamba lake lilitoa mazao maridhawa. Hii ni kwa sababu mzee huyo alizingatia mbinu bora za kilimo.
Shamba la mzee huyo lilipakana na msitu mkubwa. Msituni humo mlikuwa na wanyama wa kila aina kuanzia nyani, paa, mbogo na tembo. Kila mara wanyama hao walitaka kuvamia shamba la Mzee Mati. Hata hivyo, aliwafukuzilia mbali ili kulinda mali yake.
Mazao yalipokomaa, mzee huyo alikuwa akivuna na kubakisha mazao kiasi shambani. Kuanzia hapo, hakuwazuia wanyama tena kuingia shambani. Waliingia na kutoka walivyotaka.
Nyani walikerwa sana na mzee huyo. Walishindwa kuelewa kwa nini alivuna yale mazao mazuri kwanza kisha akawaachia kidogo tu. Wakati mmoja, Mzee Mati alishikwa na ugonjwa akazidiwa kabisa. Nyani waliandaa sherehe kubwa kusherehekea hali hiyo. Mzee alizidi kuugua kwa muda mrefu akashindwa kushiriki shughuli zozote shambani. Msimu wa mavuno ulipofika wanyama walienda shambani kama kawaida lakini walikaribishwa na magugu pekee. “Kumbe baniani mbaya kiatu chake dawa,” Nyani mmoja alisema kwa masikitiko.
Wanyama walikuja kugundua kuwa Mzee Mati ambaye walimchukulia kama adui alikuwa msaada mkubwa kwao. Tangu hapo walimwombea kila siku ili aweze kupona na kuendelea na shughuli zake. Mungu si Athumani. Mzee alianza kupata nafuu.
4. Andika funzo moja linalojitokeza katika hadithi hii. (alama 1)
Answer
Tusiwadharau watu wanaotusaidia hata kama msaada wao ni mdogo, kwa sababu baniani mbaya kiatu chake dawa.
Wanyama walimwona Mzee Mati kama adui, lakini alipougua walikosa chakula, wakajua kuwa alikuwa msaada mkubwa kwao.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Uzalendo ni nini? (alama 1)Question 5
- Mzalendo hufanya mambo yote haya isipokuwaQuestion 6
- Andika njia moja ambayo wewe binafsi unaweza kuonyesha uzalendo. (alama 1)Question 7
- Neno 'nia' limetumika katika kifungu. Kisawe cha neno hilo niQuestion 8
- Andika habari kuu iliyoangaziwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Question 9
- Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 10. (alama 1)Question 10