CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 37
Hatufai kukata tamaa kwa sababu ya changamoto za maisha. Jadili kauli hii ukirejelea mfano wa mamaye Subira. (alama 2)
From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
NOVELA
Soma dondoo ifuatayo kisha ujibu maswali.
Subira alisimama pale mbele ya hadhira kubwa akipokea shahada yake ya uzamili. Machozi yalimdondoka ndo ndo ndo! Alisikia akimiminiwa sifa kochokocho kwa weledi wake masomoni. Utawala wa chuo kikuu hicho cha Umma University ulimtambua kwa ubunifu wake uliokifanya chuo hicho kijulikane kitaifa na kimataifa.
Alitembea taratibu akapokea kipazasauti. Akaanza, “Wenzangu, safari yangu haikuwa rahisi. Ilianza kule kijijini Kajificheni. Wazazi wangu walikuwa watu na vyao. Walimiliki shamba kubwa la mibuni. Mimi na wazazi wangu tuliishi kwa furaha mithili ya mfalme katika kasri yake.
Mauti hayana huruma. Maskini baba aliugua uele wa saratani. Kifo kilitutembelea usiku mmoja kikaondoka na maskini baba yangu. Ami zetu hawakukawia kutuonyesha lango la mji wa baba. Tulihamia mjini ambapo mama alishiriki biashara ndogondogo na kuwafulia watu nguo nyumbani.
Mungu si Athumani, kipato kidogo alichopata mama kilikidhi mahitaji yetu. Katu sikuwa kupe masomoni. Nilitia chudi nikapata matokeo bora katika mitihani mbalimbali. Mwishowe, niliomba ufadhili katika shirika moja la kijamii. Msaada huo umeniongoza katika safari yangu ya elimu hadi hapa nilipo.
Ninapoiona shahada hii, ninakumbuka juhudi za mama yangu. Ninaona ndoto ya mashirika ya kijamii yanayowathamini wanafunzi kutoka familia zisizo na uwezo wa kifedha. Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina. Ninawasihi vijana wenzangu wafuate nyayo zangu katika masomo. Asanteni sana.”
Alipohitimisha, umati ulilipuka kwa makofi. Alitembea taratibu na kumkumbatia mama yake.
Hatufai kukata tamaa kwa sababu ya changamoto za maisha. Jadili kauli hii ukirejelea mfano wa mamaye Subira. (alama 2)
Answer
Baada ya baba kufariki na ami kuwafukuza, mama hakukata tamaa: alihamia mjini akafanya biashara ndogondogo na kuwafulia watu nguo. Kipato chake kidogo kilikidhi mahitaji yao, na Subira akasoma hadi kupata shahada ya uzamili.
Mama alikabili kifo cha mumewe, kufukuzwa na umaskini, lakini juhudi zake ziliwalisha na kumwezesha Subira kusoma.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Mwandishi wa dondoo hii ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Huku ukitolea mifano mwafaka, eleza mbinu zozote tatu kati…Question 38
- Kwa nini Mzee Mati alipata mazao mengi kila msimu? (alama 1)Question 1
- Ni jambo lipi linaloonyesha kuwa Mzee Mati aliwajali wanyama? (alama 1)Question 2
- Unafikiria ni kwa nini nyani waliandaa sherehe? (alama 1)Question 3
- Andika funzo moja linalojitokeza katika hadithi hii. (alama 1)Question 4
- Uzalendo ni nini? (alama 1)Question 5