naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 34

Andika aina mbili za mandhari yanayojitokeza katika dondoo hii. (alama 2)

From Kiswahili — Term One Opener Assessment 2025 (Set 3) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela

NOVELA
Soma dondoo ifuatayo kisha ujibu maswali.

Subira alisimama pale mbele ya hadhira kubwa akipokea shahada yake ya uzamili. Machozi yalimdondoka ndo ndo ndo! Alisikia akimiminiwa sifa kochokocho kwa weledi wake masomoni. Utawala wa chuo kikuu hicho cha Umma University ulimtambua kwa ubunifu wake uliokifanya chuo hicho kijulikane kitaifa na kimataifa.

Alitembea taratibu akapokea kipazasauti. Akaanza, “Wenzangu, safari yangu haikuwa rahisi. Ilianza kule kijijini Kajificheni. Wazazi wangu walikuwa watu na vyao. Walimiliki shamba kubwa la mibuni. Mimi na wazazi wangu tuliishi kwa furaha mithili ya mfalme katika kasri yake.

Mauti hayana huruma. Maskini baba aliugua uele wa saratani. Kifo kilitutembelea usiku mmoja kikaondoka na maskini baba yangu. Ami zetu hawakukawia kutuonyesha lango la mji wa baba. Tulihamia mjini ambapo mama alishiriki biashara ndogondogo na kuwafulia watu nguo nyumbani.

Mungu si Athumani, kipato kidogo alichopata mama kilikidhi mahitaji yetu. Katu sikuwa kupe masomoni. Nilitia chudi nikapata matokeo bora katika mitihani mbalimbali. Mwishowe, niliomba ufadhili katika shirika moja la kijamii. Msaada huo umeniongoza katika safari yangu ya elimu hadi hapa nilipo.

Ninapoiona shahada hii, ninakumbuka juhudi za mama yangu. Ninaona ndoto ya mashirika ya kijamii yanayowathamini wanafunzi kutoka familia zisizo na uwezo wa kifedha. Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina. Ninawasihi vijana wenzangu wafuate nyayo zangu katika masomo. Asanteni sana.”

Alipohitimisha, umati ulilipuka kwa makofi. Alitembea taratibu na kumkumbatia mama yake.

Andika aina mbili za mandhari yanayojitokeza katika dondoo hii. (alama 2)

Answer

Ukumbi wa mahafali katika chuo kikuu cha Umma University; kijijini Kajificheni (shamba la mibuni).

Dondoo linaanza katika sherehe ya mahafali chuoni, kisha Subira anasimulia maisha yake kijijini Kajificheni na baadaye mjini.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test