CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025: KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha)
Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · 30 questions
Topics: Kusoma, Sarufi na Matumizi ya Lugha.
All 30 questions with answers
- Question 1: Wanafunzi wa Gredi ya nne walizuru mbuga gani ya wanyama?Answer: Mbuga ya Masai Mara
- Question 2: Mwelekezi anaelewa kuhusu wanyama wa pori kwa sababu:Answer: Aliwaeleza kuhusu kuhama kwa kongoni na faida za wanyama wa pori.
- Question 3: Je, unafikiri wanafunzi wa Gredi ya nne waliporudi shuleni walifanya nini?Answer: Waliwahadithia wenzao kuhusu wanyama na faida zao.
- Question 4: Ni nini maana ya neno tulizuru kulingana na kifungu?Answer: Tulitembelea
- Question 5: Ili kuishi vyema tunafaa kuzingatia nini?Answer: Afya bora
- Question 6: Kwa kurejelea ubeti wa tatu taja faida ya chakula mwilini.Answer: Huupa mwili nguvu.
- Question 7: Mtu akikosa lishe bora, atapata shida gani?Answer: Atapata maradhi.
- Question 8: Ni nini maana ya kauli, 'Akili iwe timamu?'Answer: Akili iwe sawasawa.
- Question 9: Mzee Juma aliishi katika kijiji gani?Answer: Kijiji cha Jitegemee
- Question 10: Andika sentensi kutoka kwenye hadithi, inayoonyesha kuwa Mzee Juma ni mkarimu.Answer: Hata hivyo, waliokosa pesa aliwasaidia.
- Question 11: Unafikiri wanakijiji walifanya nini baada ya kuona bidii ya Mzee Juma?Answer: Walianza kufanya kazi kwa bidii kama yeye.
- Question 12: Jina lingine la mkokoteni ni rukwama. Je, jina lingine la pesa ni ___.Answer: Fedha
- Question 13: Wanakijiji cha Tumaini walikuwa na ___ kwa muda mrefu.Answer: utulivu
- Question 14: Vijana wa kijiji cha Tumaini walibadilika vipi baada ya kushauriwa?Answer: Walianza kwenda shuleni na kuwatii watu wazima.
- Question 15: Unafikiri Bi. Maridhia alifanya nini baada ya kutuzwa?Answer: Alifurahi sana na kuendelea kuwasaidia vijana.
- Question 16: Waliandaa sherehe inamaanisha:Answer: Walitayarisha sherehe.
- Question 17: Tazama picha hizi kisha ujibu maswali. Andika ngeli za kila nomino za picha hizo kwenye jedwali hili: farasi, kiatu.Answer: farasi: A-WA; kiatu: KI-VI
- Question 18: Jaza nafasi kwa kutumia kiambishi cha wakati kinachofaa. Jana Koros alisafisha chumba chake. Sasa hivi a___fua nguo zake.Answer: anafua
- Question 19: Hassan amempata mama yake sebuleni asubuhi akamwamkua, "Shikamoo mama." Je, mama alimjibu vipi?Answer: Marahaba
- Question 20: Jedwali hili lina maneno katika hali mbalimbali. Chagua neno lililo katika hali ya ukubwa.Answer: B. jiji
- Question 21: Tazama picha hii. Maua yako kando ya runinga. Paka yuko ___Meza.Answer: chini ya
- Question 22: Nina mipira mitatu. Kila mpira umeandikwa aina mbalimbali za maneno. Chagua mpira ambao una vitenzi pekee.Answer: A. Mpira A: lima, ita, ruka
- Question 23: Andika wingi wa sentensi: Mgeni amefika kwangu leo.Answer: Wageni wamefika kwetu leo.
- Question 24: Tazama picha hii. Mpapai nilioupanda umekuwa ___ kama twiga.Answer: mrefu
- Question 25: Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi. Tina amepika chakula. Chakula ___na Tina.Answer: B. kimepikwa
- Question 26: Jaza nafasi. Fuata mfano ulio kwenye jedwali. Ninasoma kitabu sasa. → Sisomi kitabu sasa Alicheza mpira jana. → ___Answer: Hakucheza mpira jana.
- Question 27: Chagua jibu sahihi kujaza nafasi. Sara anaandika insha ___rafiki yake anafuta ubao.Answer: A. lakini
- Question 28: Chagua neno moja kukamilisha sentensi ifuatayo. ___ vimenunuliwa.Answer: B. vingi
- Question 29: Umefika katika kituo cha basi. Kabla ya kuingia garini, kondakta amekukumbusha uvae barakoa, utamwambiaje?Answer: B. asante
- Question 30: Umemtembelea rafiki yako ambaye ni mgonjwa. Je, utatamka neno gani kuonyesha unavyohisi?Answer: Pole