naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 16

Waliandaa sherehe inamaanisha:

From Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati

Swali la 13 hadi la 16
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Kijiji cha Tumaini kina wakazi wengi. Wakazi hawa wamekuwa na utulivu kwa muda mrefu. Hata hivyo, likizo iliyopita wanakijiji walilalamikia mienendo mibaya ya baadhi ya vijana. Kuna vijana ambao walivalia mavazi yasiyofaa. Kuna wale ambao walianza kukataa kwenda shuleni. Wengine hawakutii watu wazima.

Bi. Maridhia ni mmoja wa wanakijiji hiki. Alikuwa na shirika lake kwa jina, Inua Vijana. Kupitia kwa shirika hili, alitumia redio kuwaelimisha vijana kuhusu mienendo mizuri. Aliandaa siku ya michezo kijijini. Vikundi mbalimbali vilishiriki. Baada ya michezo hii, washindi walituzwa. Bi. Maridhia alitumia nafasi hii kuwashauri.

Bidii ya Bi. Maridhia ilifaulu. Vijana waliokuwa wamepotoka walibadilika. Wanakijiji walifurahi. Walitambua juhudi za Bi. Maridhia. Waliandaa sherehe kubwa. Walimtuza Bi. Maridhia kwa juhudi zake. Hakika, mcheza kwao hutuzwa.

16. Waliandaa sherehe inamaanisha:

Answer

Walitayarisha sherehe.

Kuandaa ni kutayarisha au kupanga.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test