CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 15
Unafikiri Bi. Maridhia alifanya nini baada ya kutuzwa?
From Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Swali la 13 hadi la 16
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Kijiji cha Tumaini kina wakazi wengi. Wakazi hawa wamekuwa na utulivu kwa muda mrefu. Hata hivyo, likizo iliyopita wanakijiji walilalamikia mienendo mibaya ya baadhi ya vijana. Kuna vijana ambao walivalia mavazi yasiyofaa. Kuna wale ambao walianza kukataa kwenda shuleni. Wengine hawakutii watu wazima.
Bi. Maridhia ni mmoja wa wanakijiji hiki. Alikuwa na shirika lake kwa jina, Inua Vijana. Kupitia kwa shirika hili, alitumia redio kuwaelimisha vijana kuhusu mienendo mizuri. Aliandaa siku ya michezo kijijini. Vikundi mbalimbali vilishiriki. Baada ya michezo hii, washindi walituzwa. Bi. Maridhia alitumia nafasi hii kuwashauri.
Bidii ya Bi. Maridhia ilifaulu. Vijana waliokuwa wamepotoka walibadilika. Wanakijiji walifurahi. Walitambua juhudi za Bi. Maridhia. Waliandaa sherehe kubwa. Walimtuza Bi. Maridhia kwa juhudi zake. Hakika, mcheza kwao hutuzwa.
15. Unafikiri Bi. Maridhia alifanya nini baada ya kutuzwa?
Answer
Alifurahi sana na kuendelea kuwasaidia vijana.
Baada ya kutuzwa, angefurahi na kuendelea na kazi yake nzuri.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Waliandaa sherehe inamaanisha:Question 16
- Tazama picha hizi kisha ujibu maswali. Andika ngeli za kila nomino za picha hizo kwenye jedwali hili: farasi, kiatu.Question 17
- Jaza nafasi kwa kutumia kiambishi cha wakati kinachofaa. Jana Koros alisafisha chumba chake. Sasa hivi a___fua nguo…Question 18
- Hassan amempata mama yake sebuleni asubuhi akamwamkua, "Shikamoo mama." Je, mama alimjibu vipi?Question 19
- Jedwali hili lina maneno katika hali mbalimbali. Chagua neno lililo katika hali ya ukubwa.Question 20
- Tazama picha hii. Maua yako kando ya runinga. Paka yuko ___Meza.Question 21