naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 10

Andika sentensi kutoka kwenye hadithi, inayoonyesha kuwa Mzee Juma ni mkarimu.

From Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Swali la 9 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Mapato ni kitu apatacho mtu baada ya kufanya kazi fulani. Je, unajua kuwa kuna njia mbalimbali za kujipatia mapato?

Mzee Juma, mwanakijiji cha Jitegemee alizijua njia hizi. Alishiriki katika kilimo cha mboga na matunda ya kila aina. Pia, alifuga kuku wa kutaga, beberu na pia ng'ombe wa kukamua. Wote walipatikana katika kishamba alichonunua kwa jasho lake. Mbali na hayo, aliweka akiba kutokana na shughuli zake za kilimo. Benki mbalimbali zilikubali kumpa mikopo kujiendeleza hata zaidi.

Watu wengi walimbandika jina, Karimu. Najua unastaajabu ni kwa nini. Yeye hakubagua kazi yoyote. Mara ungempata akisukuma mkokoteni aliouita 'meli,' akiwabebea wanakijiji mikungu ya ndizi, mboga na matunda hadi sokoni. Walimlipa kwa shughuli hiyo. Hata hivyo, waliokosa pesa aliwasaidia.

Hebu tazama katika kijiji chako. Utawapata walimu, madaktari, polisi na wengine katika sekta ya jua kali. Je, unafahamu kuwa hawa hufanya kazi hizi ili kujipatia mapato?

10. Andika sentensi kutoka kwenye hadithi, inayoonyesha kuwa Mzee Juma ni mkarimu.

Answer

Hata hivyo, waliokosa pesa aliwasaidia.

Mtu mkarimu huwasaidia wengine bila malipo: waliokosa pesa aliwasaidia.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test