CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 8
Ni nini maana ya kauli, 'Akili iwe timamu?'
From Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati
Swali la 5 hadi la 8
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
1. Nataja jambo muhimu, afya bora uijue,
Ni kwa kila binadamu, aketi ajifunzie,
Ashike yake nidhamu, mwili akautunzie,
Afya bora zingatia, upate kuishi vyema.
2. Akili iwe timamu, ili nasi tutulie,
Tusipate uwazimu, mabaya sifikirie,
Mazoezi kila zamu, uwanjani tufanyie,
Afya bora zingatia, upate kuishi vyema.
3. Mlo uletao hamu, na nguvu usiwachie,
Wa kujenga ni jukumu, mbali usitupilie,
Virutubisho vya humu, mwili wako upatie,
Afya bora zingatia, upate kuishi vyema.
4. La mwisho wewe fahamu, maradhi yafukuzie,
Miaka mingi utimu, matunda uyatumie,
Nyama pasipo hukumu, ulapo zifikirie,
Afya bora zingatia, upate kuishi vyema.
8. Ni nini maana ya kauli, 'Akili iwe timamu?'
Answer
Akili iwe sawasawa.
Akili timamu ni akili iliyo sawasawa, isiyo na uwazimu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Mzee Juma aliishi katika kijiji gani?Question 9
- Andika sentensi kutoka kwenye hadithi, inayoonyesha kuwa Mzee Juma ni mkarimu.Question 10
- Unafikiri wanakijiji walifanya nini baada ya kuona bidii ya Mzee Juma?Question 11
- Jina lingine la mkokoteni ni rukwama. Je, jina lingine la pesa ni ___.Question 12
- Wanakijiji cha Tumaini walikuwa na ___ kwa muda mrefu.Question 13
- Vijana wa kijiji cha Tumaini walibadilika vipi baada ya kushauriwa?Question 14