naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 1

Wanafunzi wa Gredi ya nne walizuru mbuga gani ya wanyama?

From Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Swali la 1 hadi la 4
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Sisi ni wanafunzi wa Gredi ya nne. Shule yetu inaitwa Jikazeni. Muhula uliopita tulizuru mbuga ya wanyama ya Masai Mara. Ni ziara ambayo sote tunaikumbuka.

Mbugani, tuliwaona wanyama wa kila aina. Mwalimu wetu Bwana Masengo alikuwa ametueleza kuhusu baadhi ya wanyama wa pori ambao tungewaona. Pia, alitufahamisha kuwa tungewaona kongoni ambao ni kivutio kikuu cha watalii katika mbuga ya Masai Mara. Sote tulikuwa na hamu ya kuwaona kongoni. Wengi wetu tulikuwa tumewaona wanyama hao katika runinga na vitabuni tu.

Hatimaye tuliwaona kongoni. Mwelekezi wa ziara yetu mbugani alitueleza mengi kuhusu kongoni. Alisema kuwa kongoni huhama kutoka Tanzania kwenda Kenya wakati fulani. Vilevile, alitueleza kuhusu faida za wanyama wa pori kwa taifa letu. Kwa mfano, wanyama wa pori huvutia watalii wengi nchini. Utulivu uliokuwa mbugani ulitukumbusha wimbo wa "Kenya yetu hakuna matata." Ziara hii ilitufunza kuwa, kutembea kwingi ni kuona mengi.

1. Wanafunzi wa Gredi ya nne walizuru mbuga gani ya wanyama?

Answer

Mbuga ya Masai Mara

Kifungu kinasema, "Muhula uliopita tulizuru mbuga ya wanyama ya Masai Mara."

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test