naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 14

Ni nani huwasaidia wanafunzi kuelewa masomo shuleni?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali 13 – 15.
Elimu ni ufunguo wa maisha. Inatusaidia kujifunza kusoma, kuandika na kuelewa mambo mengi yanayotuzunguka. Watoto wanapoenda shuleni, wanapata maarifa ambayo, yatawasaida baadaye maishani.
Shuleni, watoto hujifunza masomo mbalimbali kama vile Kiswahili, Hisabati, Sayansi na michezo. Pia hujifunza maadili mema kama heshima, nidhamu na kushirikiana na wengine. Mwalimu huwaongoza wanafunzi ili waweze kuelewa, vizuri na kufanya kazi kwa bidii. Kupitia elimu, tunaweza kuwa madaktari, walimu, mafundi au viongozi bora. Elimu pia hufundisha nidhamu, upendo na kuheshimiana. Ndiyo maana ni muhimu kila mtoto ahudhurie shule kila siku.

14. Ni nani huwasaidia wanafunzi kuelewa masomo shuleni?

  1. AWazazi
  2. BMarafiki
  3. CWalimu
  4. DMadaktari

Answer

C. Walimu

Mwalimu huwaongoza.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test