CBC Grade 4 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 2
Neema angemjibu Pendo vipi baada ya kusalimiwa?
From Kiswahili — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–5.
Pendo na Neema wako kwenye uwanja wa shule yao wakati wa chakula cha mchana.
Pendo: Hujambo Neema? Leo unakula chakula gani?
Neema: Nala ugali na sukumawiki. Je, wewe unakula chakula gani?
Pendo: Nala wali, nyama na mboga. Chakula chako hakina chakula cha kujenga mwili. Hebu nikugawie nyama.
Neema: Asante sana, Pendo. Samahani, mimi huwa sili nyama.
Neema angemjibu Pendo vipi baada ya kusalimiwa?
- ASijambo
- BFiti
- CMarahaba
- DNiko poa
Answer
A. Sijambo
Salamu "Hujambo?" hujibiwa kwa "Sijambo". "Marahaba" ni jibu la "Shikamoo", na "Fiti" na "Niko poa" si Kiswahili sanifu.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Neema alikuwa anakula chakula gani?Question 3
- Nyama ni chakula cha aina gani?Question 4
- Kwa nini Neema alikataa nyama aliyopewa na Pendo?Question 5
- Kauli, "Bima alikuwa kipenzi cha kila mmoja shuleni," ina maana gani?Question 6
- Bima alijihusisha na shughuli gani wakati wake wa ziada?Question 7
- Bima alikuwa akiamka wakati gani?Question 8