naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 6

Kauli, "Bima alikuwa kipenzi cha kila mmoja shuleni," ina maana gani?

From Kiswahili — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6–9.

Bima alikuwa kipenzi cha kila mmoja shuleni. Wanafunzi wengi walitaka awe rafiki yao. Alikuwa mwerevu masomoni na matokeo yake mazuri yalimfanya kutuzwa kila wanafunzi walipofanya tathmini. Tuzo alizojishindia zilimfanya aheshimiwe kote shuleni.

Alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wa kwanza kufika shuleni. Kila siku, aliamka mapema. Angetumia muda wake wa ziada kusoma vitabu vya hadithi maktabani na hata kusakura mtandaoni. Alijishindia tuzo na kupatiwa vyeti kadhaa.

Alisifiwa na walimu hadi akaanza kujigamba. Maringo yakawa mengi zaidi. Bima akaanza kuwadharau kila mmoja, wakiwemo walimu wake. Baada ya muda mfupi akaanza kuchelewa shuleni na kupiga kelele darasani. Kimasomo akaanza kudidimia na hatimaye akaacha kwenda shuleni.

Kauli, "Bima alikuwa kipenzi cha kila mmoja shuleni," ina maana gani?

  1. AAlipendwa
  2. BAlikuwa maarufu
  3. CAliheshimiwa
  4. DAlijulikana sana

Answer

A. Alipendwa

Kipenzi ni mtu anayependwa sana. Kwa hivyo, kauli hii inamaanisha kwamba Bima alipendwa na kila mtu shuleni.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test