CBC Grade 4 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 8
Bima alikuwa akiamka wakati gani?
From Kiswahili — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6–9.
Bima alikuwa kipenzi cha kila mmoja shuleni. Wanafunzi wengi walitaka awe rafiki yao. Alikuwa mwerevu masomoni na matokeo yake mazuri yalimfanya kutuzwa kila wanafunzi walipofanya tathmini. Tuzo alizojishindia zilimfanya aheshimiwe kote shuleni.
Alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wa kwanza kufika shuleni. Kila siku, aliamka mapema. Angetumia muda wake wa ziada kusoma vitabu vya hadithi maktabani na hata kusakura mtandaoni. Alijishindia tuzo na kupatiwa vyeti kadhaa.
Alisifiwa na walimu hadi akaanza kujigamba. Maringo yakawa mengi zaidi. Bima akaanza kuwadharau kila mmoja, wakiwemo walimu wake. Baada ya muda mfupi akaanza kuchelewa shuleni na kupiga kelele darasani. Kimasomo akaanza kudidimia na hatimaye akaacha kwenda shuleni.
Bima alikuwa akiamka wakati gani?
- AMchana
- BJioni
- CJua lilipochomoza
- DMapambazuko
Answer
D. Mapambazuko
Kifungu kinasema "aliamka mapema". Mapema sana asubuhi, kabla ya jua kuchomoza, ni mapambazuko.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Ni jambo gani lililosababisha matokeo ya Bima masomoni kudidimia?Question 9
- Kulingana na kifungu hiki, kuna aina ngapi za matunda yaliyotajwa?Question 10
- Dodo hapendi kula tunda gani?Question 11
- Ni tunda gani linalopendwa na Dodo, Beja na Kimo?Question 12
- Kwa nini kilimo hutegemewa?Question 13
- Ni wakati gani ambapo mkulima huwa na kazi ngumu?Question 14