CBC Grade 4 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 13
Kwa nini kilimo hutegemewa?
From Kiswahili — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13–15.
Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu. Ukulima hapa nchini ndiyo kazi yenye mategemeo makubwa kwa maisha ya mwanadamu. Uhai wa mwanadamu hutegemea lishe bora. Karibu kila sehemu ya nchi hii ina wakulima wa kutosha. Ardhi yetu pia ina rutuba.
Ingawa kilimo kinahitaji uvumilivu wa kutosha, ndiyo kazi ambayo wananchi wameitegemea zaidi. Kazi ngumu katika kilimo huwa wakati wa kutayarisha shamba. Yawezekana msitu wenyewe ni mgumu. Zana za kukatia lazima zinolewe na kuwa na makali ya kutosha. Ardhi yenye msitu huweza kuchomwa ili kuhakikisha kuwa ardhi tosha ya upanzi imepatikana.
Kwa kawaida, utemaji wa msitu hufanywa wakati wa kiangazi hasa jua linapokuwa kali. Hii ni kwa sababu shamba linatakiwa likauke sana ili lichomeke kabisa.
Muda mfupi kabla ya mvua, mbegu hupandwa. Pindi mvua inaponyesha, mmea hustawi na kunawiri vilivyo. Kukiwa na ukame, mmea hunyauka na hata kukauka kabisa. Hii huwa hasara kubwa kwa mkulima.
Kwa nini kilimo hutegemewa?
- AArdhi ya kilimo ni kubwa
- BUhai wetu hutegemea lishe bora
- CKila sehemu ya nchi ina wakulima wa kutosha
- DKilimo kina faida kubwa
Answer
B. Uhai wetu hutegemea lishe bora
Kifungu kinasema kilimo ni kazi yenye mategemeo makubwa kwa maisha kwa sababu "uhai wa mwanadamu hutegemea lishe bora".