CBC Grade 4 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 15
Mkulima hupata hasara kubwa wakati gani?
From Kiswahili — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13–15.
Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu. Ukulima hapa nchini ndiyo kazi yenye mategemeo makubwa kwa maisha ya mwanadamu. Uhai wa mwanadamu hutegemea lishe bora. Karibu kila sehemu ya nchi hii ina wakulima wa kutosha. Ardhi yetu pia ina rutuba.
Ingawa kilimo kinahitaji uvumilivu wa kutosha, ndiyo kazi ambayo wananchi wameitegemea zaidi. Kazi ngumu katika kilimo huwa wakati wa kutayarisha shamba. Yawezekana msitu wenyewe ni mgumu. Zana za kukatia lazima zinolewe na kuwa na makali ya kutosha. Ardhi yenye msitu huweza kuchomwa ili kuhakikisha kuwa ardhi tosha ya upanzi imepatikana.
Kwa kawaida, utemaji wa msitu hufanywa wakati wa kiangazi hasa jua linapokuwa kali. Hii ni kwa sababu shamba linatakiwa likauke sana ili lichomeke kabisa.
Muda mfupi kabla ya mvua, mbegu hupandwa. Pindi mvua inaponyesha, mmea hustawi na kunawiri vilivyo. Kukiwa na ukame, mmea hunyauka na hata kukauka kabisa. Hii huwa hasara kubwa kwa mkulima.
Mkulima hupata hasara kubwa wakati gani?
- AMsimu wa mvua nyingi
- BMimea inapochipuka
- CWakati wa kutayarisha shamba
- DWakati wa ukame
Answer
D. Wakati wa ukame
Kukiwa na ukame, mimea hunyauka na kukauka kabisa. Kifungu kinasema hii huwa hasara kubwa kwa mkulima.