CBC Grade 4 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 7
Bima alijihusisha na shughuli gani wakati wake wa ziada?
From Kiswahili — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6–9.
Bima alikuwa kipenzi cha kila mmoja shuleni. Wanafunzi wengi walitaka awe rafiki yao. Alikuwa mwerevu masomoni na matokeo yake mazuri yalimfanya kutuzwa kila wanafunzi walipofanya tathmini. Tuzo alizojishindia zilimfanya aheshimiwe kote shuleni.
Alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wa kwanza kufika shuleni. Kila siku, aliamka mapema. Angetumia muda wake wa ziada kusoma vitabu vya hadithi maktabani na hata kusakura mtandaoni. Alijishindia tuzo na kupatiwa vyeti kadhaa.
Alisifiwa na walimu hadi akaanza kujigamba. Maringo yakawa mengi zaidi. Bima akaanza kuwadharau kila mmoja, wakiwemo walimu wake. Baada ya muda mfupi akaanza kuchelewa shuleni na kupiga kelele darasani. Kimasomo akaanza kudidimia na hatimaye akaacha kwenda shuleni.
Bima alijihusisha na shughuli gani wakati wake wa ziada?
- AAlipiga kelele darasani
- BAliwatembelea marafiki
- CAlisoma vitabu vya hadithi na kusakura mtandaoni
- DAlicheza na wenzake
Answer
C. Alisoma vitabu vya hadithi na kusakura mtandaoni
Kifungu kinasema angetumia muda wake wa ziada kusoma vitabu vya hadithi maktabani na hata kusakura mtandaoni.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Bima alikuwa akiamka wakati gani?Question 8
- Ni jambo gani lililosababisha matokeo ya Bima masomoni kudidimia?Question 9
- Kulingana na kifungu hiki, kuna aina ngapi za matunda yaliyotajwa?Question 10
- Dodo hapendi kula tunda gani?Question 11
- Ni tunda gani linalopendwa na Dodo, Beja na Kimo?Question 12
- Kwa nini kilimo hutegemewa?Question 13