CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 6
Chagua jibu lililo sahihi kulingana na aya ya kwanza:
From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Kifungu: Paka na Panya
Hapo zamani za kale, paka na panya waliishi kwa amani na ushirikiano mkubwa nyumbani kwa binadamu. Walimsaidia kufanya kazi ndogondogo hapo nyumbani. Binadamu naye aliwathamini kwa kuwapa mahitaji yao ya kimsingi kama vile chakula, makazi na mavazi.
Siku moja, binadamu alikuwa na wageni mashuhuri nyumbani mwake. Aliwaandalia wageni wale pilau tamu, mboga na kitoweo cha kuku. Chakula hicho kilinukia vizuri kiasi cha kuwavutia hata watu waliokuwa wakipita barabarani.
Wageni walipofika, mpishi aliitwa awaletee chakula mezani. Lo! Nyama ya kuku ilipofunuliwa, iligunduliwa kuwa ilikuwa imetafunwa tafunwa na kubakiza mifupa tu. Ilibidi mpishi arudi jikoni haraka kuandaa kitoweo kingine. Binadamu aliwaita paka na panya kwa hasira akaanza kuwagombeza. Panya alishikilia kwa viapo kuwa alimwona paka akila mnofu ule wa nyama. Katika hali hiyo, paka alipewa adhabu kali ya kutokula chakula chochote kwa siku mbili.
Walipokuwa wakiondoka, ghafla kipande cha nyama ya kuku kilianguka kutoka mfukoni mwa suruali ya panya. Wageni walishangazwa sana na tamaa pamoja na udanganyifu wa panya. Paka naye alitimua mbio ghafla akitaka kumkamata na kumadhibu. Hata hivyo, panya alikimbilia shimoni akajificha humo. Mpaka leo hii, panya hukimbilia shimoni mara tu amwonapo paka au binadamu. Yeye hutoka kisirisiri kuiba chakula wakati ambapo haonekani.

- APaka alikuwa akiishi kando na panya
- BBinadamu aliwasaidia paka na panya kufanya kazi zao
- CBinadamu ndiye aliyewapa paka na panya mahitaji yao
- DPaka alimsaidia binadamu huku panya akipumzika tu
Answer
C. Binadamu ndiye aliyewapa paka na panya mahitaji yao
Jibu sahihi ni C. Aya ya kwanza inasema binadamu aliwathamini paka na panya "kwa kuwapa mahitaji yao ya kimsingi kama vile chakula, makazi na mavazi." Chaguo A si sahihi kwa sababu wote waliishi nyumbani kwa binadamu, wala si kando. Chaguo B na D zimegeuza ukweli: paka na panya ndio waliomsaidia binadamu kufanya kazi ndogondogo.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Ipi si sifa ya panya kulingana na kifungu hiki?Question 7
- Ni jambo lipi linaloonyesha ukatili au dhuluma kwa wanyama kulingana na kifungu hiki?Question 8
- Kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki ni:Question 9
- Chagua jibu sahihi kulingana na maelezo ya aya ya kwanza:Question 10
- Manufaa makuu ya shughuli za vikundi kulingana na kifungu hiki ni kuwa:Question 11
- Mwanafunzi hawezi kufanikiwa masomoni bila kushirikiana na wenzake. Methali zifuatazo zinaweza kutumika kurejelea…Question 12