CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 5
Neno "zaraa" jinsi lilivyotumika katika mazungumzo lina maana sawa na:
From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Mazungumzo kati ya Chacha na Mawia
(Chacha anazungumza na rafiki yake Mawia.)
Chacha: Je, ungependa kufanya kazi gani baada ya kukamilisha masomo yako?
Mawia: Ningependa sana kuwa rubani. Marubani hulipwa mshahara mzuri sana na hawachoki kwa kufanya kazi ngumu. Je, wewe ungependelea kuwa nani?
Chacha: Ninatamani sana kuwa mkulima. Nalipenda sana somo la zaraa.
Mawia: (Akishangaa) Ala! Ukulima ni kazi kweli? Unataka kuishi ukiwa mchafu? Ukulima sio kazi nzuri hata kidogo.
Chacha: Kwa nini unasema si kazi nzuri?
Mawia: Kazi hiyo inachosha sana. Aidha, wakulima wengi ni maskini hohehahe.
Chacha: Hapo sikubaliani nawe kabisa, ndugu yangu. Ukulima ni kazi kama nyingine yoyote. Wapo wakulima wenye mali nyingi hata kuliko viongozi wakuu serikalini.
Mawia: (Akiwa na shauku) Enhee! Hebu nieleze zaidi, rafiki yangu.
Chacha: Mkulima mzuri huwekeza kwa kununua pembejeo za kilimo. Anaweza kununua mitambo ya kulima, kupalilia, kuvuna na hata kunyunyizia dawa. Sio lazima asagike kwenye mpini wa jembe kila siku.
Chacha: Si hayo tu, ukitumia mbinu za kisasa za kilimo, unaweza kujiongezea kipato kikubwa bila hata kuwa na shamba kubwa. Teknolojia mpya imechangia kuvumbuliwa kwa mbegu zinazostahimili ukame na vimelea. Kwa hivyo, mkulima huhakikishiwa mazao bora wakati wote.
Mawia: Kumbe! Nimekuwa na mtazamo tofauti sana kuhusu kilimo. Sasa umenifumbua macho. Sasa nakuunga mkono kikamilifu. Nimegundua kuwa una maarifa ya kutosha kuhusu kilimo.

- Ashamba
- Bmavuno
- Ckilimo
- Dmimea
Answer
C. kilimo
Jibu sahihi ni C. Chacha anasema anapenda "somo la zaraa", kisha mazungumzo yote yanahusu ukulima na kilimo. Zaraa ni neno la Kiarabu lenye maana ya kilimo. Shamba ni mahali ambapo kilimo hufanyika, mavuno ni mazao yanayovunwa na mimea ni viumbe vinavyopandwa, kwa hiyo hayo si maana ya "zaraa" kama somo.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu lililo sahihi kulingana na aya ya kwanza:Question 6
- Ipi si sifa ya panya kulingana na kifungu hiki?Question 7
- Ni jambo lipi linaloonyesha ukatili au dhuluma kwa wanyama kulingana na kifungu hiki?Question 8
- Kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki ni:Question 9
- Chagua jibu sahihi kulingana na maelezo ya aya ya kwanza:Question 10
- Manufaa makuu ya shughuli za vikundi kulingana na kifungu hiki ni kuwa:Question 11