naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 11

Manufaa makuu ya shughuli za vikundi kulingana na kifungu hiki ni kuwa:

From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Kifungu kuhusu shughuli za vikundi
Mwanafunzi hawezi kufanikiwa kimasomo bila kushirikiana kikamilifu na wenzake. Hii ndiyo sababu mwalimu huwapanga wanafunzi katika vikundi mbalimbali ili wabadilishane maarifa. Ni muhimu ieleweke kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kudai kwamba anajua kila kitu. Hata wale wanaoonekana kuwa werevu sana darasani hawakosi mambo wasiyoyajua.

Vilevile, yule mwanafunzi anayepuuzwa au kuonekana mnyonge anaweza kutoa mchango mkubwa ambao utakifaa sana kikundi chake.

Shughuli hizi za vikundi husaidia kuimarisha maadili mbalimbali miongoni mwa wanafunzi. Mathalani, heshima na upendo hukuzwa mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wengine na kuwarekebisha kwa upendo bila kuwadhalilisha wala kuwacheka. Hii ni njia nzuri sana ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa tangu utotoni.

Manufaa makuu ya shughuli za vikundi kulingana na kifungu hiki ni kuwa:

  1. Ahuwafanya wanafunzi wadhalilishane darasani
  2. Bbaadhi ya wanafunzi hupuuzwa na kuachwa nyuma
  3. Chukuza maadili mema na mshikamano wa kitaifa
  4. Dhuwaondolea walimu kazi ngumu ya kufundisha

Answer

C. hukuza maadili mema na mshikamano wa kitaifa

Jibu sahihi ni C. Aya ya mwisho inasema shughuli za vikundi "husaidia kuimarisha maadili mbalimbali", kama heshima na upendo, na ni njia ya "kuimarisha mshikamano wa kitaifa tangu utotoni." Chaguo A, B na D ni mambo mabaya au yasiyotajwa, na kifungu hakivitaji kama manufaa.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test