CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 12
Mwanafunzi hawezi kufanikiwa masomoni bila kushirikiana na wenzake. Methali zifuatazo zinaweza kutumika kurejelea ujumbe huu ipasavyo ISIPOKUWA:
From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Mwanafunzi hawezi kufanikiwa kimasomo bila kushirikiana kikamilifu na wenzake. Hii ndiyo sababu mwalimu huwapanga wanafunzi katika vikundi mbalimbali ili wabadilishane maarifa. Ni muhimu ieleweke kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kudai kwamba anajua kila kitu. Hata wale wanaoonekana kuwa werevu sana darasani hawakosi mambo wasiyoyajua.
Vilevile, yule mwanafunzi anayepuuzwa au kuonekana mnyonge anaweza kutoa mchango mkubwa ambao utakifaa sana kikundi chake.
Shughuli hizi za vikundi husaidia kuimarisha maadili mbalimbali miongoni mwa wanafunzi. Mathalani, heshima na upendo hukuzwa mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wengine na kuwarekebisha kwa upendo bila kuwadhalilisha wala kuwacheka. Hii ni njia nzuri sana ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa tangu utotoni.
Mwanafunzi hawezi kufanikiwa masomoni bila kushirikiana na wenzake. Methali zifuatazo zinaweza kutumika kurejelea ujumbe huu ipasavyo ISIPOKUWA:
- AMgaagaa na upwa hali wali mkavu
- BUpweke ni uvundo
- CMkataa wengi ni mchawi
- DJifya moja haliinjiki chungu
Answer
A. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
Jibu sahihi ni A. Ujumbe wa kifungu ni kwamba watu wanahitaji ushirikiano. "Upweke ni uvundo" na "Jifya moja haliinjiki chungu" zinaonyesha kuwa mtu peke yake hawezi kufanya mambo makubwa, na "Mkataa wengi ni mchawi" inaonya dhidi ya kukataa kushirikiana na wengine. "Mgaagaa na upwa hali wali mkavu" inamaanisha kuwa anayekaa karibu na chanzo cha riziki hapati shida; haihusu ushirikiano, kwa hiyo ndiyo isiyofaa.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Ni mji upi uliotembelewa na wanafunzi wengi zaidi kulingana na jedwali?Question 13
- Ni nani aliyewahi kutembelea miji mingi zaidi kuliko wenzake wote?Question 14
- Jedwali hili limechunguza ziara za wanafunzi katika miji mingapi tofauti?Question 15
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (16).Question 16
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (17).Question 17
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (18).Question 18