CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 10
Chagua jibu sahihi kulingana na maelezo ya aya ya kwanza:
From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Kifungu kuhusu shughuli za vikundi
Mwanafunzi hawezi kufanikiwa kimasomo bila kushirikiana kikamilifu na wenzake. Hii ndiyo sababu mwalimu huwapanga wanafunzi katika vikundi mbalimbali ili wabadilishane maarifa. Ni muhimu ieleweke kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kudai kwamba anajua kila kitu. Hata wale wanaoonekana kuwa werevu sana darasani hawakosi mambo wasiyoyajua.
Vilevile, yule mwanafunzi anayepuuzwa au kuonekana mnyonge anaweza kutoa mchango mkubwa ambao utakifaa sana kikundi chake.
Shughuli hizi za vikundi husaidia kuimarisha maadili mbalimbali miongoni mwa wanafunzi. Mathalani, heshima na upendo hukuzwa mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wengine na kuwarekebisha kwa upendo bila kuwadhalilisha wala kuwacheka. Hii ni njia nzuri sana ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa tangu utotoni.

- AHakuna mwanafunzi anayejua mambo mengi kuliko wenzake
- BKila mwanafunzi huwa na mchango muhimu katika kikundi chake
- CWanafunzi wengine hawana manufaa yoyote katika vikundi vyao
- DShughuli za vikundi huwapotezea wanafunzi wakati mwingi darasani
Answer
B. Kila mwanafunzi huwa na mchango muhimu katika kikundi chake
Jibu sahihi ni B. Aya ya kwanza inasema mwanafunzi hawezi kufanikiwa bila wenzake, na kwamba hakuna mtu anayejua kila kitu hata kama ni mwerevu; kwa hiyo kila mwanafunzi anahitaji kushirikiana na wenzake, na kila mmoja ana mchango wake (jambo hili pia linasemwa wazi katika aya ya pili). Chaguo A si kweli kwa sababu aya inasema hakuna anayejua kila kitu, si kwamba wote wanalingana. Chaguo C na D zinapingana na kifungu.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Manufaa makuu ya shughuli za vikundi kulingana na kifungu hiki ni kuwa:Question 11
- Mwanafunzi hawezi kufanikiwa masomoni bila kushirikiana na wenzake. Methali zifuatazo zinaweza kutumika kurejelea…Question 12
- Ni mji upi uliotembelewa na wanafunzi wengi zaidi kulingana na jedwali?Question 13
- Ni nani aliyewahi kutembelea miji mingi zaidi kuliko wenzake wote?Question 14
- Jedwali hili limechunguza ziara za wanafunzi katika miji mingapi tofauti?Question 15
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (16).Question 16