naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 9

Kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki ni:

From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Kifungu: Paka na Panya
Hapo zamani za kale, paka na panya waliishi kwa amani na ushirikiano mkubwa nyumbani kwa binadamu. Walimsaidia kufanya kazi ndogondogo hapo nyumbani. Binadamu naye aliwathamini kwa kuwapa mahitaji yao ya kimsingi kama vile chakula, makazi na mavazi.

Siku moja, binadamu alikuwa na wageni mashuhuri nyumbani mwake. Aliwaandalia wageni wale pilau tamu, mboga na kitoweo cha kuku. Chakula hicho kilinukia vizuri kiasi cha kuwavutia hata watu waliokuwa wakipita barabarani.

Wageni walipofika, mpishi aliitwa awaletee chakula mezani. Lo! Nyama ya kuku ilipofunuliwa, iligunduliwa kuwa ilikuwa imetafunwa tafunwa na kubakiza mifupa tu. Ilibidi mpishi arudi jikoni haraka kuandaa kitoweo kingine. Binadamu aliwaita paka na panya kwa hasira akaanza kuwagombeza. Panya alishikilia kwa viapo kuwa alimwona paka akila mnofu ule wa nyama. Katika hali hiyo, paka alipewa adhabu kali ya kutokula chakula chochote kwa siku mbili.

Walipokuwa wakiondoka, ghafla kipande cha nyama ya kuku kilianguka kutoka mfukoni mwa suruali ya panya. Wageni walishangazwa sana na tamaa pamoja na udanganyifu wa panya. Paka naye alitimua mbio ghafla akitaka kumkamata na kumadhibu. Hata hivyo, panya alikimbilia shimoni akajificha humo. Mpaka leo hii, panya hukimbilia shimoni mara tu amwonapo paka au binadamu. Yeye hutoka kisirisiri kuiba chakula wakati ambapo haonekani.

Kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki ni:

  1. AWageni Nyumbani
  2. BKitoweo cha Kuku
  3. CUlafi wa Panya
  4. DWanyama Watundu

Answer

C. Ulafi wa Panya

Jibu sahihi ni C. Kichwa kizuri hueleza jambo kuu la hadithi. Hadithi hii inahusu panya mlafi aliyeiba nyama ya kuku akamsingizia paka, kwa hiyo "Ulafi wa Panya" ndicho kichwa kinachofaa zaidi. "Wageni Nyumbani" na "Kitoweo cha Kuku" ni mambo madogo tu ya hadithi, na "Wanyama Watundu" haifai kwa sababu paka hakuwa mtundu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test