naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 8

Ni jambo lipi linaloonyesha ukatili au dhuluma kwa wanyama kulingana na kifungu hiki?

From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Kifungu: Paka na Panya
Hapo zamani za kale, paka na panya waliishi kwa amani na ushirikiano mkubwa nyumbani kwa binadamu. Walimsaidia kufanya kazi ndogondogo hapo nyumbani. Binadamu naye aliwathamini kwa kuwapa mahitaji yao ya kimsingi kama vile chakula, makazi na mavazi.

Siku moja, binadamu alikuwa na wageni mashuhuri nyumbani mwake. Aliwaandalia wageni wale pilau tamu, mboga na kitoweo cha kuku. Chakula hicho kilinukia vizuri kiasi cha kuwavutia hata watu waliokuwa wakipita barabarani.

Wageni walipofika, mpishi aliitwa awaletee chakula mezani. Lo! Nyama ya kuku ilipofunuliwa, iligunduliwa kuwa ilikuwa imetafunwa tafunwa na kubakiza mifupa tu. Ilibidi mpishi arudi jikoni haraka kuandaa kitoweo kingine. Binadamu aliwaita paka na panya kwa hasira akaanza kuwagombeza. Panya alishikilia kwa viapo kuwa alimwona paka akila mnofu ule wa nyama. Katika hali hiyo, paka alipewa adhabu kali ya kutokula chakula chochote kwa siku mbili.

Walipokuwa wakiondoka, ghafla kipande cha nyama ya kuku kilianguka kutoka mfukoni mwa suruali ya panya. Wageni walishangazwa sana na tamaa pamoja na udanganyifu wa panya. Paka naye alitimua mbio ghafla akitaka kumkamata na kumadhibu. Hata hivyo, panya alikimbilia shimoni akajificha humo. Mpaka leo hii, panya hukimbilia shimoni mara tu amwonapo paka au binadamu. Yeye hutoka kisirisiri kuiba chakula wakati ambapo haonekani.

Ni jambo lipi linaloonyesha ukatili au dhuluma kwa wanyama kulingana na kifungu hiki?

  1. APaka kunyimwa chakula kwa siku mbili bila hatia
  2. BPaka na panya kuishi nyumba moja na binadamu
  3. CPanya kutafunatafuna nyama ya wageni
  4. DPanya kudai kuwa alimwona paka akila mnofu

Answer

A. Paka kunyimwa chakula kwa siku mbili bila hatia

Jibu sahihi ni A. Paka alipewa adhabu kali ya kutokula kwa siku mbili ilhali hakuwa na kosa, kwa sababu panya ndiye aliyeiba nyama. Kuadhibu mnyama asiye na hatia ni dhuluma. Kuishi nyumba moja kunaonyesha amani (B). Kutafuna nyama ni kosa la panya (C), na kudai kuwa alimwona paka akila ni uongo wa panya (D); mambo hayo ni udanganyifu na ulafi, wala si ukatili wa binadamu kwa mnyama.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test