CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026: Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) (Test 12)
Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 21 questions
Topics: Kuandika, Kusoma.
All 21 questions with answers
- Question 1: SEHEMU A (Alama 15) ZOEZI LA I: INSHA Andika insha inayomalizia kwa maneno yafuatayo: “...Sitawahi kusahau usiku huo maishani.”Answer: USIKU WA MAFURIKO Ilikuwa mwezi wa Aprili, msimu wa mvua za masika. Siku hiyo mbingu zilikuwa zimetanda…
- Question 2: SEHEMU B (Alama 35) ZOEZI LA II: FASIHI SIMULIZI (Alama 10) 1. Mighani ni hadithi zinazohusu mashujaa. Tambua na ueleze aina hii ya…Answer: Ni kisasili (hadithi ya asili au ya usuli). Inaeleza chanzo au asili ya jamii ya Wakikuyu: Ngai aliwaumba…
- Question 3: Eleza mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika hadithi hii. (alama 2)Answer: Tashbihi: “Mabinti tisa waliokuwa warembo kama malkia”; uzuri wa mabinti unalinganishwa na wa malkia kwa…
- Question 4: Eleza sifa mbili za fasihi simulizi kama utanzu wa fasihi. (alama 2)Answer: Huwasilishwa kwa mdomo, ana kwa ana, mbele ya hadhira. Ni mali ya jamii nzima, si ya mtu mmoja.
- Question 5: Umepewa nafasi ya kuwasilisha hadithi hii mbele ya hadhira, je, utazingatia vipengele gani katika uwasilishaji wako? (alama 2)Answer: Nitatumia ishara za uso na mikono kuonyesha matukio, na nitapandisha na kushusha sauti ili hadhira ivutiwe.
- Question 6: Hadithi ni mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi. Taja vipera vingine viwili vya fasihi simulizi. (alama 2)Answer: Semi (kama methali na vitendawili) na ushairi simulizi (nyimbo).
- Question 7: ZOEZI LA III: NOVELA (Alama 10) 6. Bainisha aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Answer: Njiani au safarini: wasafiri wanatembea kuelekea mpakani Gera, wakisoma mabango ya umbali. Msituni: asubuhi…
- Question 8: Eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika sehemu hii ya novela. (alama 4)Answer: Tashbihi: “tulikuwa na matumaini kama ya tai”; matumaini yao yanalinganishwa na ya tai kwa kutumia “kama”.…
- Question 9: Eleza mfuatano wa matukio mawili makuu yaliyojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Answer: Kwanza, wasafiri walitembea kimya kuelekea Gera, na msimulizi akakumbuka kisa cha Waisraeli akaomba dua…
- Question 10: Tambua suala kuu linalojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 1)Answer: Ukimbizi: watu wanatoroka kwa miguu kuelekea mpakani Gera ili kujiokoa.
- Question 11: Eleza sifa mbili za msimulizi katika sehemu hii ya novela. (alama 1)Answer: Ni mcha Mungu: aliomba dua fupi ili Mungu awanusuru. Ni mvumilivu: licha ya uchovu alikaza mwendo.
- Question 12: ZOEZI LA IV: TAMTHILIA (Alama 10) 11. Mandhari ni kipengele muhimu katika kazi ya fasihi. Tambua mandhari katika sehemu hii ya tamthilia.…Answer: Ni nyumbani kwa Mabula na Mishi, mtaani Madongoporomoka, usiku wa manane.
- Question 13: Eleza sifa mbili za tamthilia kwa kurejelea sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)Answer: Imeandikwa kwa mazungumzo kati ya wahusika, Mishi na Mabula. Ina maelekezo ya jukwaa kwenye mabano, k.m.…
- Question 14: Mbinu za lugha hutumiwa na mwandishi ili kuongeza ladha katika kazi yake. Tambua na ueleze mbinu mbili za lugha katika sehemu hii ya…Answer: Methali: Mishi anasema “mazoea yana taabu”, kuonyesha kuwa ni vigumu kuacha tabia uliyoizoea. Kando: “(Kama…
- Question 15: Maudhui ni masuala makuu katika kazi ya fasihi. Eleza masuala mawili yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)Answer: Ulevi: Mabula anakunywa vileo vya visachet na kurudi nyumbani usiku wa manane. Umaskini: Mabula na Mishi…
- Question 16: Fasihi ni kioo cha jamii. Eleza mambo mawili ambayo yameangaziwa katika sehemu hii ya tamthilia na yameonekana katika ulimwengu wa…Answer: Kukatika au kupunguzwa kwa umeme usiku, jambo linalotokea katika miji yetu. Kupanda kwa bei ya umeme na…
- Question 17: ZOEZI LA V: USHAIRI (Alama 5) 16. Shairi hili ni la aina gani? Eleza. (alama 1)Answer: Ni tarbia, kwa sababu kila ubeti una mishororo minne.
- Question 18: Tambua vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu. (alama 1)Answer: Vina vya kati ni -ni (punguzeni, zigaweni, nchini, tuzindukeni) na vina vya mwisho ni -ie (situmie, zibakie).
- Question 19: Tambua wahusika wawili katika shairi hili. (alama 1)Answer: Mshairi (nafsi neni) na Wakenya.
- Question 20: Tambua ujumbe katika shairi hili. (alama 1)Answer: Taka zisitupwe ovyo bali zipunguzwe, zitenganishwe na kutumiwa kama malighafi ya kuleta faida.
- Question 21: Tambua idadi ya mizani katika ubeti wa mwisho. (alama 1)Answer: Kila mshororo una mizani 16 (8 katika ukwapi na 8 katika utao), hivyo ubeti wa mwisho una mizani 64.