naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 6

Hadithi ni mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi. Taja vipera vingine viwili vya fasihi simulizi. (alama 2)

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 2 marks · Topic: Kusoma, Fasihi Simulizi

Soma fasihi simulizi ifuatayo kisha ujibu maswali.

Jamii ya Wakikuyu huamini kuwa Mungu, Ngai, ndiye muumba na chanzo cha uhai wao. Mungu alimuumba Gikuyu na Mkewe Mumbi, wazazi wa kwanza wa jamii ya Wakikuyu.

Siku moja Ngai aliwatokea Gikuyu na Mumbi na kuwapatia shamba lililokuwa kusini magharibi mwa Mlima Kenya, yaani Kirinyaga. Gikuyu alijenga nyumba mahali palipoitwa Mukurwe wa Nyagathanga, Murang'a. Mahali hapa hadi leo huaminika kuwa patakatifu na pana miti mingi ya migumo. Pametambulika na kutengwa kama eneo la hifadhi ya utamaduni wa Wakikuyu.

Gikuyu na Mumbi walijaliwa Mabinti tisa waliokuwa warembo kama malkia. Mabinti hawa ni pamoja na; Wanjiru, Wambui, Njeri, Wanjiku, Nyambura, Wairimu, Waithera, Wangari na Wangui. Mabinti hawa walipobaleghe na kuwa tayari kuozwa, Gikuyu alitoa kafara na kumwomba Ngai chini ya mti wa mugumo.

Siku iliyofuata, wanaume tisa walitokea chini ya mti huo. Wanaume hao ndio waliowaoa mabinti wa Gikuyu na Mumbi. Familia hizo tisa zikawa ndizo koo za Wakikuyu.

5. Hadithi ni mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi. Taja vipera vingine viwili vya fasihi simulizi. (alama 2)

Answer

Semi (kama methali na vitendawili) na ushairi simulizi (nyimbo).

Mbali na hadithi, fasihi simulizi ina semi (methali, vitendawili, nahau), ushairi simulizi au nyimbo, maigizo (michezo ya kuigiza) na mazungumzo (kama hotuba).

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test