CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 7
ZOEZI LA III: NOVELA (Alama 10) 6. Bainisha aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Gera ilikuwa umbali wa kilomita mia mbili kutoka eneo tulilokuwa. Hatukujua kama tungefika siku gani lakini tulikuwa na matumaini kama ya tai kuwa tungefika. Mara kwa mara tulisoma mabango yaliyoonyesha umbali uliokuwa umebaki kufika mpakani Gera.
Ilikuwa nadra kuona watu wakizungumza. Kila mmoja alijinyamazia zi! Ni kana kwamba kila mmoja alikuwa katika ulimwengu wake wa mawazo. Kila mmoja alisema na Mola wake. Nilikumbuka hadithi aliyotufundisha mwalimu wetu wa somo la Dini. Alikuwa ametueleza jinsi Waisraeli walivyofuatwa nyuma na jeshi la Misri ili kuwaangamiza. Alitueleza kwamba kama si kwa msaada wa Mungu kuwaokoa basi wangeangamizwa wote. Nilipokumbuka kisa hicho, niliomba dua fupi ili Mungu atunusuru kama alivyowanusuru Waisraeli. Sikutaka tupatwe na janga lolote. “Mungu tukumbuke,” hivyo ndivyo nilivyoomba sala yangu fupi.
Kwa kuwa hayakuwa mazoea yangu ya kupiga milundi, safari ilinilemea kila wakati. Nilitaka kupumzika kidogo lakini hakukuwa na muda wa kufanya hivyo. Nilikuwa na uchovu mwingi mwilini. Mama alitanabahi nimebaki nyuma wakati mmoja. Nilimwona akiniangalia huku na kule kwa wasiwasi mwingi. Alininyoosha kidole cha shahada aliponiona hatimaye. Macho yake yalinikemea. Nilichapua miguu na kukaza mwendo, moyoni nilijisemea, polepole ndio mwendo.
Ilikuwa safari ndefu. Asubuhi jua lilichomoza. Tuliendelea safari kwenye msitu wa nyika. Tuliamua kupumzika mara tulipochoka.
ZOEZI LA III: NOVELA (Alama 10)
6. Bainisha aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)
Answer
Njiani au safarini: wasafiri wanatembea kuelekea mpakani Gera, wakisoma mabango ya umbali. Msituni: asubuhi waliendelea na safari kwenye msitu wa nyika.
Mandhari ni mahali au wakati matukio yanapotokea. Hapa ni njiani kuelekea mpaka wa Gera, msitu wa nyika, na pia wakati wa usiku na asubuhi jua lilipochomoza.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika sehemu hii ya novela. (alama 4)Question 8
- Eleza mfuatano wa matukio mawili makuu yaliyojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Question 9
- Tambua suala kuu linalojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 1)Question 10
- Eleza sifa mbili za msimulizi katika sehemu hii ya novela. (alama 1)Question 11
- ZOEZI LA IV: TAMTHILIA (Alama 10) 11. Mandhari ni kipengele muhimu katika kazi ya fasihi. Tambua mandhari katika…Question 12
- Eleza sifa mbili za tamthilia kwa kurejelea sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)Question 13