CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 13
Eleza sifa mbili za tamthilia kwa kurejelea sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
Soma sehemu ya tamthilia kisha ujibu maswali.
SEHEMU I
ONYESHO III
(Usiku wa manane. Mishi ameketi. Mara anasikia matiti ya mtu anayetembea. Mishi anaonyesha wasiwasi. Mara mlango unabishwa.)
Mishi: Tendo?
Mabula: Tendo mke wangu. Kila mtu ana uwezo wa kufikiri ovu lakini maovu tuyaonayo ni ya watendao. (Anamkaribia. Hoja hii imemzuzua Mishi. Anajaribu kufikiria.) Wanielewa mke wangu? Unaona? Ni hoja kama hizi ambazo huvitoa vinywaji mfukoni mwa watu bila kupenda kwao. Kisha nikija nyumbani unafikiri nimeharibu pesa kununulia vileo. (Kama mwenye kujisemea. Kando) Hata si vile vya maana. Ni hivi visachet vilivyohalalishwa na waheshimiwa wabunge kwa ajili yetu sisi kina yakhe. (Ghafla mwangaza unapungua chumbani.) Hawa watu wa stima hawaishi kupunguza umeme usiku tunapouhitaji.
Mishi: Umeme?
Mabula: Huoni mwangaza ulivyofifia? Sasa wataongeza gharama ya umeme. Watasingizia ukame.
Mishi: (Kwa mshangao!) Mabula!
Mabula: Watasema maji yamepungua sana katika ule mto mkubwa.
Mishi: Wanasema mazoea yana taabu. Bado mpaka leo hii hazijatoka ndoto za kuishi huko kwenye maisha ya Kizungu. Huelewi kuwa tuko Madongoporomoka! (Anachukua mshumaa na kuuwasha)
Mabula: Kweli! Watasema ni gharama kubwa kufuatia kupanda kwa mafuta ya dizeli Uarabuni. Watasema wanaokoa jahazi. Watasema viwanda lazima viendelee kuzalisha mtu mnyonge asikose chakula na ajira.
12. Eleza sifa mbili za tamthilia kwa kurejelea sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)
Answer
Imeandikwa kwa mazungumzo kati ya wahusika, Mishi na Mabula. Ina maelekezo ya jukwaa kwenye mabano, k.m. “(Usiku wa manane. Mishi ameketi…)”.
Tamthilia huandikwa ili iigizwe: ina dayalojia, maelekezo ya jukwaa, migawanyo ya sehemu na maonyesho, na majina ya wahusika kabla ya maneno yao.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Mbinu za lugha hutumiwa na mwandishi ili kuongeza ladha katika kazi yake. Tambua na ueleze mbinu mbili za lugha katika…Question 14
- Maudhui ni masuala makuu katika kazi ya fasihi. Eleza masuala mawili yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia.…Question 15
- Fasihi ni kioo cha jamii. Eleza mambo mawili ambayo yameangaziwa katika sehemu hii ya tamthilia na yameonekana katika…Question 16
- ZOEZI LA V: USHAIRI (Alama 5) 16. Shairi hili ni la aina gani? Eleza. (alama 1)Question 17
- Tambua vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu. (alama 1)Question 18
- Tambua wahusika wawili katika shairi hili. (alama 1)Question 19