naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 14

Mbinu za lugha hutumiwa na mwandishi ili kuongeza ladha katika kazi yake. Tambua na ueleze mbinu mbili za lugha katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia

Soma sehemu ya tamthilia kisha ujibu maswali.

SEHEMU I
ONYESHO III

(Usiku wa manane. Mishi ameketi. Mara anasikia matiti ya mtu anayetembea. Mishi anaonyesha wasiwasi. Mara mlango unabishwa.)

Mishi: Tendo?

Mabula: Tendo mke wangu. Kila mtu ana uwezo wa kufikiri ovu lakini maovu tuyaonayo ni ya watendao. (Anamkaribia. Hoja hii imemzuzua Mishi. Anajaribu kufikiria.) Wanielewa mke wangu? Unaona? Ni hoja kama hizi ambazo huvitoa vinywaji mfukoni mwa watu bila kupenda kwao. Kisha nikija nyumbani unafikiri nimeharibu pesa kununulia vileo. (Kama mwenye kujisemea. Kando) Hata si vile vya maana. Ni hivi visachet vilivyohalalishwa na waheshimiwa wabunge kwa ajili yetu sisi kina yakhe. (Ghafla mwangaza unapungua chumbani.) Hawa watu wa stima hawaishi kupunguza umeme usiku tunapouhitaji.

Mishi: Umeme?

Mabula: Huoni mwangaza ulivyofifia? Sasa wataongeza gharama ya umeme. Watasingizia ukame.

Mishi: (Kwa mshangao!) Mabula!

Mabula: Watasema maji yamepungua sana katika ule mto mkubwa.

Mishi: Wanasema mazoea yana taabu. Bado mpaka leo hii hazijatoka ndoto za kuishi huko kwenye maisha ya Kizungu. Huelewi kuwa tuko Madongoporomoka! (Anachukua mshumaa na kuuwasha)

Mabula: Kweli! Watasema ni gharama kubwa kufuatia kupanda kwa mafuta ya dizeli Uarabuni. Watasema wanaokoa jahazi. Watasema viwanda lazima viendelee kuzalisha mtu mnyonge asikose chakula na ajira.

13. Mbinu za lugha hutumiwa na mwandishi ili kuongeza ladha katika kazi yake. Tambua na ueleze mbinu mbili za lugha katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)

Answer

Methali: Mishi anasema “mazoea yana taabu”, kuonyesha kuwa ni vigumu kuacha tabia uliyoizoea. Kando: “(Kama mwenye kujisemea. Kando) Hata si vile vya maana”; Mabula anasema jambo ambalo Mishi hasikii.

Mbinu nyingine ni nahau (wanaokoa jahazi), takriri (neno “Watasema” limerudiwa mara nyingi) na swali la balagha (Huoni mwangaza ulivyofifia?).

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test