naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 20

Tambua ujumbe katika shairi hili. (alama 1)

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

1.
Taka ni kama laana, mabaki yenye madhara,
Japo pia ni dafina, yenye na wingi ubora,
Wajua taka hazina! Iliyojaa tijara?
Wakenya tuzindukeni, taka sasa ni mtaji.

2.
Taka Kenya zimejaa, punde zaleta gharama
Maganda 'metapakaa, wa mjini walalama,
Plastiki zimezaga, gilasi na pia chuma,
Wakenya tuzindukeni, taka taleta hasara.

3.
Taka sasa punguzeni, ovyo vitu situmie,
Tena taka zigaweni, kando kando zibakie,
Iwe mradi nchini, vifaa tuzindue,
Wakenya tuzindukeni, taka iwe malighafi.

4.
Taka malighafi kaka, taka mali dada yangu
Yatoa gesi mwafaka, kupika wali na change
Bidhaaze utamaka, kapu, mikufu na vyungu,
Wakenya tuzindukeni, taka itupe faida.

19. Tambua ujumbe katika shairi hili. (alama 1)

Answer

Taka zisitupwe ovyo bali zipunguzwe, zitenganishwe na kutumiwa kama malighafi ya kuleta faida.

Mshairi anawahimiza Wakenya kuona taka kama mtaji: zinaweza kuleta gesi ya kupikia na bidhaa kama kapu, mikufu na vyungu.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test