CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 21
Tambua idadi ya mizani katika ubeti wa mwisho. (alama 1)
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
1.
Taka ni kama laana, mabaki yenye madhara,
Japo pia ni dafina, yenye na wingi ubora,
Wajua taka hazina! Iliyojaa tijara?
Wakenya tuzindukeni, taka sasa ni mtaji.
2.
Taka Kenya zimejaa, punde zaleta gharama
Maganda 'metapakaa, wa mjini walalama,
Plastiki zimezaga, gilasi na pia chuma,
Wakenya tuzindukeni, taka taleta hasara.
3.
Taka sasa punguzeni, ovyo vitu situmie,
Tena taka zigaweni, kando kando zibakie,
Iwe mradi nchini, vifaa tuzindue,
Wakenya tuzindukeni, taka iwe malighafi.
4.
Taka malighafi kaka, taka mali dada yangu
Yatoa gesi mwafaka, kupika wali na change
Bidhaaze utamaka, kapu, mikufu na vyungu,
Wakenya tuzindukeni, taka itupe faida.
20. Tambua idadi ya mizani katika ubeti wa mwisho. (alama 1)
Answer
Kila mshororo una mizani 16 (8 katika ukwapi na 8 katika utao), hivyo ubeti wa mwisho una mizani 64.
Mfano: Ta-ka-ma-li-gha-fi-ka-ka (8), ta-ka-ma-li-da-da-ya-ngu (8) = 16. Mishororo yote minne ina mizani 16 kila mmoja, jumla 64.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- SEHEMU A (Alama 15) ZOEZI LA I: INSHA Andika insha inayomalizia kwa maneno yafuatayo: “...Sitawahi kusahau usiku huo…Question 1
- SEHEMU B (Alama 35) ZOEZI LA II: FASIHI SIMULIZI (Alama 10) 1. Mighani ni hadithi zinazohusu mashujaa. Tambua na…Question 2
- Eleza mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika hadithi hii. (alama 2)Question 3
- Eleza sifa mbili za fasihi simulizi kama utanzu wa fasihi. (alama 2)Question 4
- Umepewa nafasi ya kuwasilisha hadithi hii mbele ya hadhira, je, utazingatia vipengele gani katika uwasilishaji wako?…Question 5
- Hadithi ni mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi. Taja vipera vingine viwili vya fasihi simulizi. (alama 2)Question 6