CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 3
Eleza mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika hadithi hii. (alama 2)
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 2 marks · Topic: Kusoma, Fasihi Simulizi
Soma fasihi simulizi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Jamii ya Wakikuyu huamini kuwa Mungu, Ngai, ndiye muumba na chanzo cha uhai wao. Mungu alimuumba Gikuyu na Mkewe Mumbi, wazazi wa kwanza wa jamii ya Wakikuyu.
Siku moja Ngai aliwatokea Gikuyu na Mumbi na kuwapatia shamba lililokuwa kusini magharibi mwa Mlima Kenya, yaani Kirinyaga. Gikuyu alijenga nyumba mahali palipoitwa Mukurwe wa Nyagathanga, Murang'a. Mahali hapa hadi leo huaminika kuwa patakatifu na pana miti mingi ya migumo. Pametambulika na kutengwa kama eneo la hifadhi ya utamaduni wa Wakikuyu.
Gikuyu na Mumbi walijaliwa Mabinti tisa waliokuwa warembo kama malkia. Mabinti hawa ni pamoja na; Wanjiru, Wambui, Njeri, Wanjiku, Nyambura, Wairimu, Waithera, Wangari na Wangui. Mabinti hawa walipobaleghe na kuwa tayari kuozwa, Gikuyu alitoa kafara na kumwomba Ngai chini ya mti wa mugumo.
Siku iliyofuata, wanaume tisa walitokea chini ya mti huo. Wanaume hao ndio waliowaoa mabinti wa Gikuyu na Mumbi. Familia hizo tisa zikawa ndizo koo za Wakikuyu.
2. Eleza mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika hadithi hii. (alama 2)
Answer
Tashbihi: “Mabinti tisa waliokuwa warembo kama malkia”; uzuri wa mabinti unalinganishwa na wa malkia kwa kutumia neno “kama”.
Mbinu ya lugha hutajwa na kuelezwa kwa mfano kutoka hadithini. Mfano mwingine ni orodha au taja (majina ya mabinti tisa yanaorodheshwa).
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Eleza sifa mbili za fasihi simulizi kama utanzu wa fasihi. (alama 2)Question 4
- Umepewa nafasi ya kuwasilisha hadithi hii mbele ya hadhira, je, utazingatia vipengele gani katika uwasilishaji wako?…Question 5
- Hadithi ni mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi. Taja vipera vingine viwili vya fasihi simulizi. (alama 2)Question 6
- ZOEZI LA III: NOVELA (Alama 10) 6. Bainisha aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Question 7
- Eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika sehemu hii ya novela. (alama 4)Question 8
- Eleza mfuatano wa matukio mawili makuu yaliyojitokeza katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Question 9