CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 16
Ni michezo gani haichezwi wakati wa maonyesho?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi la 17.
Kila mwaka jijini Mawengo huwa na maonyesho ya zaraa. Maonyesho ya zaraa huwa ni sherehe ya wiki moja. Katika sherehe hii watu huonyeshwa mazao na kilimo ya aina zote zinazostawi katika nchi yetu. Pia huleta mifugo wa aina kama vile: Kuku, mabatabukini, mabatamzinga, nguruwe, sungura, kondoo, mbuzi, ng'ombe na farasi.
Pamoja na mazao ya kilimo kuna vishamba vidogo vya mimea mbalimbali. Madhumuni ni kutoa vielelezo vya kilimo bora cha mimea inayohusika. Penye kila kishamba huwekwa mwalimu wa uzoefu mwingi. Huyu mwalimu hueleza ukuzaji wa mimea inayolimika, hatua kwa hatua, huku akitumia mimea yenyewe kama vifaa. Haya mafunzo yanawaelezea wakulima wazi zaidi hasa wasiojua kusoma wala kuandika.
Kuna siku mbili muhimu sana za maonyesho haya ya kilimo. Siku hizi mbili ni siku ya kufungua maonyesho na siku ya kufunga.
Katika siku ya kufunguliwa maonyesho, wageni wengi mashuhuri huhudhuria. Mheshimiwa Rais hufungua maonyesho, baadaye huwatolea raia wote na wageni hotuba ya pongezi kwa maendeleo na mafanikio yaliyopatikana.
Katika siku ya kufunga maonyesho kunaalikwa wageni kama vile Waziri wa kilimo, Mifugo au Uvuvi na Waziri wa Uendawi na Rasilimali. Mgeni huyu pia hutoa hotuba ya pongezi na shime.
Pamoja na sehemu za biashara, ufundi na kilimo huwa na maonyesho ya tamasha na ngoma za tamaduni mbalimbali. Pia huwa na maonyesho ya stadi mbalimbali kama vile kukimbia kwa farasi, kulenga shabaha kwa mishale, mikuki na kuruka kwa ndege huku wanahewa wakifanya maajabu angani. Wazimamoto pia huonyesha uhodari wao kwa kuzima moto na kuokoa watu wakati wa moto.
Maonyesho ya kilimo ni ya maana sana kwa sababu yanawafundisha watu wote wanaohudhuria mambo mengi yanayohusu kilimo, biashara, ufundi na starehe.
16. Ni michezo gani haichezwi wakati wa maonyesho?
- AKukimbia kwa farasi
- BKulenga shabaha
- CKandanda
- DKuruka kwa ndege
Answer
C. Kandanda
Kifungu kinataja kukimbia kwa farasi, kulenga shabaha na kuruka kwa ndege; kandanda (mpira wa miguu) haitajwi.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ni kichwa gani mwafaka kwa kifungu hiki?Question 17
- Ni vyakula gani hupunguzwa bei kwa pamoja siku ya Jumanne na Jumapili?Question 18
- Ni vyakula vipi havipunguzwi bei siku za wikendi?Question 19
- Kwa jumla, ni aina ngapi za vyakula hazipunguzwi bei hata mara moja wikendi?Question 20
- Chagua jibu sahihi kukamilisha nafasi ya 21 iliyoachwa wazi kwenye kifungu.Question 21
- Ni nini ambacho kinaonyesha kuwa mazungumzo kati ya Baraka na Nyanya ni ya mahojiano?Question 22