naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 22

Ni nini ambacho kinaonyesha kuwa mazungumzo kati ya Baraka na Nyanya ni ya mahojiano?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.

(Baraka yuko nyumbani. Ameamka na kukutana na Nyanya)

Nyanya: (Akitabasamu) Umeamkaje bwana yangu?

Baraka: (Akifunika uso kwa viganja vyake) Vizuri. Shikamoo.

Nyanya: ___21___ (wakitazamana ana kwa ana) Kwa nini unafunika uso?

Baraka: Mimi si bwana yako.

Nyanya: (Akicheka kwa sauti kweli) Wewe si ni somo ya marehemu mume wangu? Mnafanana naye kama shilingi kwa ya pili.

Baraka: Babu ni somo yangu kweli.

Nyanya: Sasa unanikana tena mtani wangu? Niambie.

Baraka: (Kwa ujasiri) Sikukani nyanya.

Nyanya: Uso wenyewe! Kwa nini hujanawa uso?

Baraka: (anaona haya. Anaweka mikono pamoja na kuinamisha kichwa) Samahani nyanya. Nitanawa.

Nyanya: Haya nenda ukanawe uso kwanza kisha uje nikupe uji.

22. Ni nini ambacho kinaonyesha kuwa mazungumzo kati ya Baraka na Nyanya ni ya mahojiano?

  1. AMmoja wao anajibu maswali.
  2. BWana mjadala.
  3. CWanazingatia kiimbo.
  4. DWanakatana kalima.

Answer

A. Mmoja wao anajibu maswali.

Nyanya anauliza maswali (Kwa nini unafunika uso? Kwa nini hujanawa uso?) na Baraka anayajibu: hayo ni mahojiano.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test