CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 21
Chagua jibu sahihi kukamilisha nafasi ya 21 iliyoachwa wazi kwenye kifungu.
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.
(Baraka yuko nyumbani. Ameamka na kukutana na Nyanya)
Nyanya: (Akitabasamu) Umeamkaje bwana yangu?
Baraka: (Akifunika uso kwa viganja vyake) Vizuri. Shikamoo.
Nyanya: ___21___ (wakitazamana ana kwa ana) Kwa nini unafunika uso?
Baraka: Mimi si bwana yako.
Nyanya: (Akicheka kwa sauti kweli) Wewe si ni somo ya marehemu mume wangu? Mnafanana naye kama shilingi kwa ya pili.
Baraka: Babu ni somo yangu kweli.
Nyanya: Sasa unanikana tena mtani wangu? Niambie.
Baraka: (Kwa ujasiri) Sikukani nyanya.
Nyanya: Uso wenyewe! Kwa nini hujanawa uso?
Baraka: (anaona haya. Anaweka mikono pamoja na kuinamisha kichwa) Samahani nyanya. Nitanawa.
Nyanya: Haya nenda ukanawe uso kwanza kisha uje nikupe uji.
21. Chagua jibu sahihi kukamilisha nafasi ya 21 iliyoachwa wazi kwenye kifungu.
- AMarahaba
- BSijambo
- CAlamsiki
- DMakiwa
Answer
A. Marahaba
Baraka amemsalimu Nyanya kwa “Shikamoo”, na jibu la shikamoo ni “Marahaba”.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ni nini ambacho kinaonyesha kuwa mazungumzo kati ya Baraka na Nyanya ni ya mahojiano?Question 22
- Ni salamu gani ingefaa wakati wa asubuhi?Question 23
- Nyanya anamweleza Baraka kuwa “Mnafanana naye kama shilingi kwa ya pili” Je, hii ni mbinu gani ya lugha?Question 24
- Ni viziada lugha gani ambavyo Baraka ametumia kuonyesha hali ya kuona haya?Question 25
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 27.Question 27