naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 25

Ni viziada lugha gani ambavyo Baraka ametumia kuonyesha hali ya kuona haya?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.

(Baraka yuko nyumbani. Ameamka na kukutana na Nyanya)

Nyanya: (Akitabasamu) Umeamkaje bwana yangu?

Baraka: (Akifunika uso kwa viganja vyake) Vizuri. Shikamoo.

Nyanya: ___21___ (wakitazamana ana kwa ana) Kwa nini unafunika uso?

Baraka: Mimi si bwana yako.

Nyanya: (Akicheka kwa sauti kweli) Wewe si ni somo ya marehemu mume wangu? Mnafanana naye kama shilingi kwa ya pili.

Baraka: Babu ni somo yangu kweli.

Nyanya: Sasa unanikana tena mtani wangu? Niambie.

Baraka: (Kwa ujasiri) Sikukani nyanya.

Nyanya: Uso wenyewe! Kwa nini hujanawa uso?

Baraka: (anaona haya. Anaweka mikono pamoja na kuinamisha kichwa) Samahani nyanya. Nitanawa.

Nyanya: Haya nenda ukanawe uso kwanza kisha uje nikupe uji.

25. Ni viziada lugha gani ambavyo Baraka ametumia kuonyesha hali ya kuona haya?

  1. AKuweka mikono usoni
  2. BKucheka kwa sauti
  3. CKutazamana ana kwa ana.
  4. DKutabasamu.

Answer

A. Kuweka mikono usoni

Baraka alifunika uso kwa viganja vyake na kuweka mikono pamoja huku akiinamisha kichwa: ishara za kuona haya.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test