CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 41
Habari hii inatudokeza kuwa
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari kisha ujibu maswali 34 - 43.
Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni. Aliamini rafiki zake walimwonea gere Maulid, na kwamba hawakupenda afanikiwe katika jambo lolote. Alipomaliza kazi jioni hiyo, alikwenda kumkabidhi mwanawe leseni aliyonunua Bomani. Alimwelezea mwanawe ajihadhari na watu wabaya waliojaribu kumharibia maisha yake. Alisema babamtu, “Jihadhari na watu wa aina ya ndumakuwili. Kama humfahamu, ndumakuwili ni kama nyoka. Huyu ndumakuwili ana sumu baridi huuma akivuvia. Hana mkia yeye; ana vichwa pande zote mbili. Mwanangu, duniani humu mna watu sawasawa na ndumakuwili. Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa. Njama zao kutambaa na maovu yao huzagaa. Huuma wakipuliza afanyavyo huyo manyama. Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae. Liga ikiisha kukuingia mwanangu, ndivyo hivyo tena......!”
41. Habari hii inatudokeza kuwa
- Ahakuna nyoka aitwaye ndumakuwili.
- Bwatu hao hawata-mbai lakini njama zao huenea jinsi ambavyo nyoka hao hutambaa kuenezea sumu zao.
- Cwatu hawa ni watu nao nyoka hao ni nyoka lakini tabia zao ni sawa; kueneza sumu.
- Dmtu ana kichwa kimoja ilhali ndumakwili ana mkia miwili.
Answer
B. watu hao hawata-mbai lakini njama zao huenea jinsi ambavyo nyoka hao hutambaa kuenezea sumu zao.
"Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa": njama zao huenea kama nyoka anavyotambaa.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Mwisho mwisho msomaji anamwonya na kumtadharisha mwanae ajihadhari na kujitenga na wabayaQuestion 42
- Lengo la taarifa hii hasa ni kutoa taadhari kuhusu hulka za binadamu waovu pamoja na kutoaQuestion 43
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 44.Question 44
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 45.Question 45
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 46.Question 46
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 47.Question 47