CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 40
Tabia mbaya sana ya mtu ndumakuwili ni
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari kisha ujibu maswali 34 - 43.
Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni. Aliamini rafiki zake walimwonea gere Maulid, na kwamba hawakupenda afanikiwe katika jambo lolote. Alipomaliza kazi jioni hiyo, alikwenda kumkabidhi mwanawe leseni aliyonunua Bomani. Alimwelezea mwanawe ajihadhari na watu wabaya waliojaribu kumharibia maisha yake. Alisema babamtu, “Jihadhari na watu wa aina ya ndumakuwili. Kama humfahamu, ndumakuwili ni kama nyoka. Huyu ndumakuwili ana sumu baridi huuma akivuvia. Hana mkia yeye; ana vichwa pande zote mbili. Mwanangu, duniani humu mna watu sawasawa na ndumakuwili. Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa. Njama zao kutambaa na maovu yao huzagaa. Huuma wakipuliza afanyavyo huyo manyama. Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae. Liga ikiisha kukuingia mwanangu, ndivyo hivyo tena......!”
40. Tabia mbaya sana ya mtu ndumakuwili ni
- Aunafiki
- Burafiki
- Cunadilifu
- Dubadhirifu
Answer
A. unafiki
Ndumakuwili ni mnafiki: ana "vichwa pande zote mbili".
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Habari hii inatudokeza kuwaQuestion 41
- Mwisho mwisho msomaji anamwonya na kumtadharisha mwanae ajihadhari na kujitenga na wabayaQuestion 42
- Lengo la taarifa hii hasa ni kutoa taadhari kuhusu hulka za binadamu waovu pamoja na kutoaQuestion 43
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 44.Question 44
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 45.Question 45
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 46.Question 46