naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 39

Baba mtu anatuambia kwamba

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma habari kisha ujibu maswali 34 - 43.
Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni. Aliamini rafiki zake walimwonea gere Maulid, na kwamba hawakupenda afanikiwe katika jambo lolote. Alipomaliza kazi jioni hiyo, alikwenda kumkabidhi mwanawe leseni aliyonunua Bomani. Alimwelezea mwanawe ajihadhari na watu wabaya waliojaribu kumharibia maisha yake. Alisema babamtu, “Jihadhari na watu wa aina ya ndumakuwili. Kama humfahamu, ndumakuwili ni kama nyoka. Huyu ndumakuwili ana sumu baridi huuma akivuvia. Hana mkia yeye; ana vichwa pande zote mbili. Mwanangu, duniani humu mna watu sawasawa na ndumakuwili. Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa. Njama zao kutambaa na maovu yao huzagaa. Huuma wakipuliza afanyavyo huyo manyama. Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae. Liga ikiisha kukuingia mwanangu, ndivyo hivyo tena......!”

39. Baba mtu anatuambia kwamba

  1. Awatu ndumakuwili ni wapika majungu.
  2. Bwapika majungu ni ndumakuwili.
  3. Cwatu hujifanya wema machoni kumbe ndumakuwili wapika majungu.
  4. Dukiwa na mtoto wako watu watamwonea gere.

Answer

C. watu hujifanya wema machoni kumbe ndumakuwili wapika majungu.

Ndumakuwili huonekana wema lakini maneno yao ya uovu hutambaa.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test