naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 35

Taarifa hii inatufahamisha kuwa

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma habari kisha ujibu maswali 34 - 43.
Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni. Aliamini rafiki zake walimwonea gere Maulid, na kwamba hawakupenda afanikiwe katika jambo lolote. Alipomaliza kazi jioni hiyo, alikwenda kumkabidhi mwanawe leseni aliyonunua Bomani. Alimwelezea mwanawe ajihadhari na watu wabaya waliojaribu kumharibia maisha yake. Alisema babamtu, “Jihadhari na watu wa aina ya ndumakuwili. Kama humfahamu, ndumakuwili ni kama nyoka. Huyu ndumakuwili ana sumu baridi huuma akivuvia. Hana mkia yeye; ana vichwa pande zote mbili. Mwanangu, duniani humu mna watu sawasawa na ndumakuwili. Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa. Njama zao kutambaa na maovu yao huzagaa. Huuma wakipuliza afanyavyo huyo manyama. Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae. Liga ikiisha kukuingia mwanangu, ndivyo hivyo tena......!”

35. Taarifa hii inatufahamisha kuwa

  1. Amsemaji hakuwapenda rafikize.
  2. Bmsemaji hakumwamini mwanawe.
  3. Cmsemaji anashuku mwanawe aonewa kijicho.
  4. Dmsemaji ana mwana bora sana wa kutokewa mfano.

Answer

C. msemaji anashuku mwanawe aonewa kijicho.

Aliamini rafiki walimwonea gere (kijicho) mwanawe.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test