CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 34
Msemaji wa habari hii amepata fedhaa zaidi
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari kisha ujibu maswali 34 - 43.
Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni. Aliamini rafiki zake walimwonea gere Maulid, na kwamba hawakupenda afanikiwe katika jambo lolote. Alipomaliza kazi jioni hiyo, alikwenda kumkabidhi mwanawe leseni aliyonunua Bomani. Alimwelezea mwanawe ajihadhari na watu wabaya waliojaribu kumharibia maisha yake. Alisema babamtu, “Jihadhari na watu wa aina ya ndumakuwili. Kama humfahamu, ndumakuwili ni kama nyoka. Huyu ndumakuwili ana sumu baridi huuma akivuvia. Hana mkia yeye; ana vichwa pande zote mbili. Mwanangu, duniani humu mna watu sawasawa na ndumakuwili. Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa. Njama zao kutambaa na maovu yao huzagaa. Huuma wakipuliza afanyavyo huyo manyama. Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae. Liga ikiisha kukuingia mwanangu, ndivyo hivyo tena......!”
34. Msemaji wa habari hii amepata fedhaa zaidi
- Akwa kutahadharishwa na ndumakuwili.
- Bkutokana na mwanawe kuitwa mhuni.
- Caliponunua leseni kutoka Bomani.
- Dalipojua mwanawe hawezi kufanikiwa.
Answer
B. kutokana na mwanawe kuitwa mhuni.
"Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni."