CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 36
Kwa mujibu wa habari hii, mzazi anamtaka mwanawe
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari kisha ujibu maswali 34 - 43.
Geshum alifadhaishwa sana na mwanawe kuitwa mhuni. Aliamini rafiki zake walimwonea gere Maulid, na kwamba hawakupenda afanikiwe katika jambo lolote. Alipomaliza kazi jioni hiyo, alikwenda kumkabidhi mwanawe leseni aliyonunua Bomani. Alimwelezea mwanawe ajihadhari na watu wabaya waliojaribu kumharibia maisha yake. Alisema babamtu, “Jihadhari na watu wa aina ya ndumakuwili. Kama humfahamu, ndumakuwili ni kama nyoka. Huyu ndumakuwili ana sumu baridi huuma akivuvia. Hana mkia yeye; ana vichwa pande zote mbili. Mwanangu, duniani humu mna watu sawasawa na ndumakuwili. Ingawa wao hawatambui, lakini maneno yao hutambaa. Njama zao kutambaa na maovu yao huzagaa. Huuma wakipuliza afanyavyo huyo manyama. Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae. Liga ikiisha kukuingia mwanangu, ndivyo hivyo tena......!”
36. Kwa mujibu wa habari hii, mzazi anamtaka mwanawe
- Aaendelee na masomo.
- Baende Bomani kuchukua leseni.
- Casiwe na rafiki.
- Datumie busara kuwajua watu wabaya.
Answer
D. atumie busara kuwajua watu wabaya.
"Endapo huna busara, hutatambua hadi sumu ikujae."
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Habari hii inasema kwambaQuestion 37
- Wanaofananishwa hapa na ndumakuwili niQuestion 38
- Baba mtu anatuambia kwambaQuestion 39
- Tabia mbaya sana ya mtu ndumakuwili niQuestion 40
- Habari hii inatudokeza kuwaQuestion 41
- Mwisho mwisho msomaji anamwonya na kumtadharisha mwanae ajihadhari na kujitenga na wabayaQuestion 42