CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 12
Andika kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki.
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho
UFUPISHO.
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 9 hadi la 12.
Nchi yetu imetunukiwa maliasili ya aina mbalimbali. Kati ya rasilimali hizo ni maanguko ya maji, mito, bahari, maziwa, milima, mabonde na wanyama kama vile ndovu, nyati, fisi, simba, duma na wengine wengi. Tunapaswa kuyatunza maliasili haya na kuyatumia kwa uwajibikaji ili taifa letu liweze kuimarika kiuchumi.
Inasikitisha kuona kwamba bado tunaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kutokana na ukosefu wa viwanda. Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache kutegemea za kwingine. Manufaa ya elimu ni chungu nzima.
Mwito wangu ni kuwa tufikirie namna tunavyoweza kujiendeleza kwa rasilimali zetu wenyewe. Tukiendelea na tabia yetu ya kukopa na kuomba misaada kutoka kwingine tutaishi kuwa hohehahe bila ya kuwa na mbele wala nyuma. Tunaweza kuondoa uhitaji wetu kabisa tukiutambua umuhimu wa rasilimali zetu tulizo nazo na kuzitumia kwa njia yenye manufaa.
12) Andika kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki.
Answer
Matumizi Bora ya Maliasili
Kifungu kizima kinahusu kutunza na kutumia rasilimali zetu wenyewe vizuri ili tujiendeleze bila kutegemea wengine.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 14.Question 14
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 15.Question 15
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 16.Question 16
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 17.Question 17
- Kadi zifuatazo zina nomino za aina mbalimbali. Chagua kadi yenye nomino za kawaida pekee.Question 18