CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 11
Andika ujumbe uliokolezwa rangi katika aya ya mwisho kwa sentensi moja. Ujumbe uliokolezwa rangi ni: "Tukiendelea na tabia yetu ya kukopa na kuomba misaada…
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho
UFUPISHO.
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 9 hadi la 12.
Nchi yetu imetunukiwa maliasili ya aina mbalimbali. Kati ya rasilimali hizo ni maanguko ya maji, mito, bahari, maziwa, milima, mabonde na wanyama kama vile ndovu, nyati, fisi, simba, duma na wengine wengi. Tunapaswa kuyatunza maliasili haya na kuyatumia kwa uwajibikaji ili taifa letu liweze kuimarika kiuchumi.
Inasikitisha kuona kwamba bado tunaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kutokana na ukosefu wa viwanda. Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache kutegemea za kwingine. Manufaa ya elimu ni chungu nzima.
Mwito wangu ni kuwa tufikirie namna tunavyoweza kujiendeleza kwa rasilimali zetu wenyewe. Tukiendelea na tabia yetu ya kukopa na kuomba misaada kutoka kwingine tutaishi kuwa hohehahe bila ya kuwa na mbele wala nyuma. Tunaweza kuondoa uhitaji wetu kabisa tukiutambua umuhimu wa rasilimali zetu tulizo nazo na kuzitumia kwa njia yenye manufaa.
11) Andika ujumbe uliokolezwa rangi katika aya ya mwisho kwa sentensi moja.
Ujumbe uliokolezwa rangi ni: "Tukiendelea na tabia yetu ya kukopa na kuomba misaada kutoka kwingine tutaishi kuwa hohehahe bila ya kuwa na mbele wala nyuma. Tunaweza kuondoa uhitaji wetu kabisa tukiutambua umuhimu wa rasilimali zetu tulizo nazo na kuzitumia kwa njia yenye manufaa."
Answer
Tukiacha kukopa na kutumia vizuri rasilimali zetu wenyewe, tutamaliza umaskini nchini mwetu.
Sentensi hizi mbili zinasema kwamba kutegemea mikopo na misaada kunatufanya maskini, lakini kujitegemea kwa rasilimali zetu kutaondoa uhitaji.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Andika kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki.Question 12
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 14.Question 14
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 15.Question 15
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 16.Question 16
- Chagua jibu linalofaa kujaza pengo la 17.Question 17